KAULI YA WIZARA YA ELIMU BAADA YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KUTISHIA KUANDAMANA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, December 16, 2019

KAULI YA WIZARA YA ELIMU BAADA YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KUTISHIA KUANDAMANA

  Malunde       Monday, December 16, 2019

 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema imepokea taarifa ya kuwepo kwa changamoto za mikopo ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha DSM (UDSM) na imeiagiza Bodi ya Mikopo na Uongozi wa Chuo kukutana na Serikali ya Wanafunzi UDSM (DARUSO) leo ili kutatua changamoto hizo.

Wizara imewataka Wanafunzi kuwa watulivu na kuendelea na masomo wakati changamoto hizo zikishughulikiwa.

Kauli ya Wizara ya Elimu imekuja kufuatia Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DSM kutishia kwenda kukusanyika katika Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), endapo saa 72 zitapita bila malalamiko yao kupatiwa ufumbuzi ikiwemo baadhi ya wanafunzi ambao ni wanufaika wa mkopo kutoingiziwa fedha.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post