JESHI LA POLISI LAONYA WAHALIFU KUTOTHUBUTU KUINGIA MITAANI SHEREHE ZA MWAKA MPYA

Na Ahmed Mahmoud Arusha

JESHI la Polisi mkoa wa Arusha, limesema Arusha sio sehemu salama wala ya kupumzikia kwa majambazi,wahalifu na Vibaka bali ni sehemu salama kwa raia wema tu.


Pia  Kamanda Jonathan Shana, ametuma salamu kwa Majambazi, wahalifu na Vibaka, kwamba sumu haionjwi na wakitaka kujaribu basi watainywa halafu watatambua uzuri wake.

Kamanda Shanna, ameyasema hayo  leo  ikiwa ni maandalizi ya kuupokea waka mpya 2020 ambao utaanza rasmi saa 6.00 usiku na kuoengeza kwamba Jeshi la polisi limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mkesha wa mwaka mpya .

Amesema Jeshi  la polisi litaendelea kufanya kazi ya kuhakikisha usalama na amani ya kudumu inaendelea kuwepo mkoani Arusha wakati wowote  na kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Kamanda,Shanna,amesem Jeshi hilo litaendelea kufanya kazi zake  bila kulala wala kupumzika na limejipanga kuimrisha doria maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu hasa nyakati za usiku kwenye maadhimisho ya kuupokea mwaka mpya2020.

Kamanda Shanna,amewahakikishia wananchi wote kwamba Arusha itakuwa shwari kipindi chote cha siku kuu na baada ya siku kuu na akawaonya Vibaka na wahalifu wengine kutafuta pa kwenda kwa kuwa Arusha hakuna nafasi hiyo.

Amelipongeza jeshi la polisi kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa kudhibiti matukio yote ya uhalifu,ujambazi na udokozi kwa kipindi chote cha mwaka mzima kuanzia January hadi Desemba 31 mwaka 2019.

Amewaambia kuwa kazi waliyoifanya tangia January mosi mwaka 2019 wanaihitimisha Desemba 31 saa 6.00 usiku  na wataanza upya kazi ya ulinzi na usalama kuanzia saa 6.01 usiku mwaka 2020


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527