DIAMOND PLATNUMZ APOKELEWA KISHUJAA KIGOMA.SHUHUDIA HAPA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, December 29, 2019

DIAMOND PLATNUMZ APOKELEWA KISHUJAA KIGOMA.SHUHUDIA HAPA

  Malunde       Sunday, December 29, 2019
Mwanamuziki Diamond Platnumz amepokelewa na mabango wakati akiwasili stesheni ya Nguruka Mkoani Kigoma katika kuadhimisha miaka yake kumi katika muziki.

Umati wa watu umejitokeza katika stesheni ya Nguruka Mkoani Kigoma wakiwa na mabango yaliyobeba jumbe mbalimbali kwa mwanamuziki huyo.

Moja ya mabango hayo lilikuwa limeandikwa “Karibu Diamond kwenu Kigoma tuijenge Kigoma, Sisi Nguruka tulishaanza ujenzi wa madarasa saba na vyoo 12. Tunaomba tuunge mkono, watoto 494 hawana pa kusoma.”

Diamond aliyeanza safari ya kuelekea Kigoma jana Desemba 28, 2019 akiwa na mashabiki wake katika treni lengo lake kubwa ni kujumuika na watu wa mkoa huo kusheherekea miaka kumi tangu kuanza muziki.

Nguruka ikiwa ndio stesheni ya kwanza unapoingia Mkoa wa Kigoma, Diamond alikutana na umati wa watu ukimsubiri.

Baada ya kuwasili eneo hilo Diamond alipanda jukwaani na kuanza kuwaimbisha wakazi hao wimbo wa Baba lao .


Hata hivyo ilifika mahali mzuka ukampanda kweli kama moja ya kibwagizo kilichopo katika wimbo huo kinachosema 'mzuka ukipanda hata nguo nitavua, nivue muone'walipoitikia mashabiki akavua fulana yake aliyokuwa ameivaa ambapo watu wake waliichukia na baadaye kumrudishiaUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post