CHAMA CHA CONSERVATIVE KINACHOONGOZWA NA BORIS JOHNSON CHAIBUKA KIDEDEA KATIKA UCHAGUZI UINGEREZA

Chama cha Conservative kimeshinda zaidi ya viti 326 vya Ubunge huku Kiongozi wa Chama hicho Boris Johnson akiwashukuru wapiga kura wa Uingereza kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo.



Waziri Mkuu Boris Jonhson amesema ushindi huo unaipa Serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya Raia wa Uingereza, Boris Johsnon na Chama chake walihitaji kupata viti 326 ili kutangazwa kuwa Washindi lakini wamepitisha idadi hiyo.

Huenda wingi huo wa kura za Wawakilishi Bungeni ukamuwezesha Borris kuufanikisha mpango wake wa Brexit na kuiondoa Uingereza kwenye EU kabla ya Mwezi wa pili Mwakani.


Ufaransa imesema ushindi wa Waziri Mkuu Boris Johnson utawezesha kutekelezwa mchakato wa Brexit kwa utaratibu mzuri. 

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesifu kinachoelekea kuwa ushindi wa chama cha Conservertive katika muktadha wa mkwamo wa mchakato wa Brexit.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post