CHADEMA Watoa wito kwa wananchi Njombe kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, December 29, 2019

CHADEMA Watoa wito kwa wananchi Njombe kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura

  Malunde       Sunday, December 29, 2019
Na Amiri kilagalila-Njombe
Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Njombe,kimetoa wito kwa wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura linalotarajia kuanza disemba 30,2019 mpaka januari 5,2020 mkoani humo.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Njombe Rose Mayemba wakati akizungumza na vyombo vya habari.

“Tunafahamu kwamba wananchi wamekatishwa tamaa sana na zoezi lililopita kwenye serikali za mitaa,wengi ile hari imekufa, lakini nitoe rai kwa wananchi wasiache wajibu wao wa kwenda kujiandikisha” alisema Rose Mayemba

Mwenyekiti Rose Mayemba amewaagiza viongozi wa chama hicho kuto kuacha kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha mara baada zoezi hilo kukamilika katika maeneo mengine ya nchi na sasa zoezi hilo linatarajia kuanza mkoani humo.

Aidha amesema kama vilivyowekwa vipaumbele vya chama hicho ikiwemo kudai tume huru ya uchaguzi,chama hicho hakitaweza kwenda kwenye uchaguzi bila ya kuwa na tume huru.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post