BITEKO AAGIZA WACHIMBAJI WAPEWE MCHANGA WENYE ALMASI

SALVATORY NTANDU
Serikali imekubaliana na Mgodi wa almasi wa Willimson Dimonds Limited (WDL) uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga  kuwapa mchanga wachimbaji wenye madini ya  almasi kuanzia disemba 22 mwaka lengo ikiwa ni kuwapa fursa wachimbaji wadogo kujipatia ajira.

Mgogoro huu umedumu kwa muda mrefu tangu mgodi huu ulipo anzishwa mwaka 1940 wachimbaji wadogo ili kuchukua mchanga huo ambao unaodhaniwa kuwa na almasi hivyo kutekelezwa kwa agizo hili ndio suluhisho la mgogoro huu.

Kauli hiyo imetolewa jana na  Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya almasi katika eneo la Maganzo wilayani Kishapu kuhusiana na uamuzi wa serikali wa kuwapatia mchanga huo.

“Serikali ya awamu ya tano imekubali kuwapatieni mchanga huu hakikisheni almasi yote itakayopatikana mnaiuza katika soko la Maganzo pasitokee mchimbaji hata mmoja akitorosha Madini haya”alisema Biteko.

Mgodi wa WDL utahakikisha unampata mdhabuni ambaye atautoa mchanga huo nje ya eneo la Mgodi ili wachimbaji wawezekupata fursa ya kutafuta madini hayo disemba 22 mwaka huu na hatua hiyo itasaidia kupunguza malalamiko ya wachimbaji wa Mwadui.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amesema Uongozi wa Mgodi wa Mwadui umekubali kujenga soko la kisasa la Almasi katika eneo la Maganzo ili serikali iwezekukusanya mapato.

“Wanunuzi wote wa almasi watapatikana hapa kikubwa wachimbaji mkipata uzeni kwenye soko hili ambalo linatambulika kisheria ukitorosha tukikukamata utachukuliwa hatua kali za kisheria”alisema Telack.

Nae mwakilishi wa  wachimbaji wadogo wa almasi kutoka Maganzo, Gregory Kibusa ameishukuru serikali kwa kuwatatulia mgoro huo ambao utatoa fursa kwao kujijenga kiuchumi kupitia madini ya alamsi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post