SERIKALI YATOA SIKU 60 KAMPUNI YA SONGORO IKAMILISHE KUUNDA BOTI YA MAFUNZO


Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditie akizindua boti ya Ukoaji iliyopo nyuma yake,Pmbeni yake upande wa Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha baharia Daktari Erick Massami na Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Chuo hicho Captain Ernest Bulamba.
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditie akitoa hotuba wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo cha baharia (DMI) jijini Dar es Salaam
Wahitimu wa Chuo cha bahari wakisubiri kutunukiwa vyeti vyao.



Na Hellen Isdory Dar es Salaam

Serikali imetoa siku 60 kwa Kampuni ya Kuunda Meli ya Songoro kukamilisha boti ya mafunzo kwa vitendo ambayo ina uwezo wa kubeba watu 180 ili ianze kazi haraka.

Akizungumza leo Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditie kwenye uzinduzi wa boti ya Uokoaji sambamba na mahafali ya 15 ya Chuo cha baharia (DMI) jijini Dar es Salaam alisema Mkandarasi huyo pesa alishapewa yote na serikali lakini hadi sasa hawajamaliza.

Mhandisi Nditie alibainisha kuwa boti hiyo ni muhimu kwa wanafunzi wanaosomea uhandisi na ubaharia hasa katika kusoma kwa Vitendo hivyo kuto kuwepo kwa wakati kunasababisha masomo yao yasifikie kiwango kizuri cha ufaulu.

“Ninazo taarifa kuwa chuo hiki kimepewa meli nzuri na mdau wa Maendeleo na nyie mmempa mkandarasi aitwaye Sorongo lakini hadi sasa hajakamilisha na inasemekana ni miezi miwili hajafika eneo la kazi naomba mumpe taarifa nataka hiyo meli ndani ya miezi miwili kuanzia sasa”,alisema.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi chuoni hapo Dkt. Ernest Bupamba alibainisha kuwa chuo hicho ni kikubwa na kinatoa mafunzo ya ubaharia kwa kiwango cha kimataifa na hadi sasa kimethibitika kimataifa katika viwango vya ubora.

“Chuo hiki ni kikubwa kwa Ukanda mzima wa Afrika na kimeweza kuwa kituo cha ubora katika ukanda wa Afrika mashariki na kusini mwa jangwa la sahara”,alisema.

Chuo hicho hadi sasa kinauwezo wa kubeba wanafunzi 693

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527