ABDUL NONDO ASHINDA RUFAA YA KESI YAKE DHIDI YA JAMHURI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, December 24, 2019

ABDUL NONDO ASHINDA RUFAA YA KESI YAKE DHIDI YA JAMHURI

  Malunde       Tuesday, December 24, 2019
Mahakama Kuu kanda ya Iringa, imemuachia huru aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Abdul Nondo, baada ya kukutwa hana hatia katika kesi ya Rufaa iliyokatwa na upande wa Jamhuri, baada ya kutoridhishwa na hukumu yake aliyoshinda mwaka 2018.Abdul Nondo ameachiwa jana Disemba 23, 2019, ambapo Mahakama imesisitiza kuwa hana hatia na kwamba hoja za rufaa za upande wa Serikali, zimeonekana kutokuwa na mashiko.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mara baada ya kushinda rufaa hiyo, Nondo amemshukuru Mungu pamoja na Mawakili wake waliosimama naye kuanzia mwanzo wa kesi hiyo, hadi leo alipoachiwa huru.

"Alhamdulilah,namshukuru Mungu sana,leo 23/12/2019 nimeshinda rufaa iliyofunguliwa na Jamhuri dhid ya maamuz ya kesi niliyoshinda Novemba 5, 2018, nawashukuru mawakili wangu Jebra Kambole na Chance Luoga, Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu(THRDC),pia Mahakama,ndugu na watanzania" ameandika Abdul Nondo.

Nondo alikuwa anakabiliwa na shtaka la kutoa taarifa za uongo kuwa alitekwa na watu wasiojulikana huku upande wa Jamhuri ukisema alijiteka mwenyewe.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post