WATU 15 WAJERUHIWA BAADA YA BASI LA ABIRIA KUFELI BREKI NA KUGONGA MAGARI 7 MOSHI


Watu 15 wamenusurika kifo baada ya breki za basi la abiria la kampuni ya Harambee kushindwa kufanya kazi na kupelekea basi hilo kupoteza uelekeo na kuyagonga magari mengine wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Salum Hamduni, amesema ajali hiyo ilitokea  jana jioni Jumanne Desemba 17, 2019 na kueleza imehusisha magari saba likiwamo basi la hilo la Harambee.

"Ni kweli kuna ajali imetokea jana jioni  eneo la Benki ya NBC, iliyopo katikati ya mji wa Moshi , majeruhi walikuwa 15 na mmoja ndiye aliyeumia sana lakini wengine walipata majeraha madogo ya kawaida na mishtuko na wakapewa  huduma ya kwanza," amesema Kamanda.

Kamanda Hamduni amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea na atatoa taarifa rasmi pindi utakapokamilika.


Tazama picha za CCTV.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post