WATAFITI WA SAYANSI WASHAURIWA KUWEKEZA KATIKA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Mkurugenzi wa Jukwaa la wadau wa kilimo ANSAF) Audax Rukonge akionyesha moja ya picha inayohusu Mabadiliko ya Tabia ya nchi

Na Hellen kwavava Dar es Salaam.
Watafiti nchini wameombwa kuisaidia jamii kwa kuja na teknolojia mpya ya mbegu kwa upande wa  chakula ya  muda mfupi na isiyo hitaji maji mengi ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo Audax Rukonge wakati kizungumza na waandishi wa wahabari kuhusiana na Mkutano wa mwaka ambao unatarajia kufanyika wiki ijayo lengo likiwa ni kuangalia  changamoto na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia ya nchi na fursa zipi zinapatikana kwenye mabadiliko hayo.
Rukonge alisema ipo haja kwa watafiti kuleta teknolojia mpya ya mbegu zitakazoendana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi ili wakulima kuweza kunufaika wakati wote hali ya hewa itakavyokuwa.
“Mabadiliko ya Tabia ya nchi haya tabiriki kuna wakati inaweza kuwa jua sana au mvua kubwa lakini  hali zote hizo wakulima wanahitaji kuendelea na kilimo hivyo watafiti wetu wanaweza kuja na teknolojia ya mbegu mbadala itakayoweza kuhimili vipindi vyote vya hali ya hewa”,alisema Rukonge.
Aidha aliongeza kwa kusema kwamba kunahitajika pia teknolojia itayowezesha wakulima kuhifadhi chakula vizuri ikiwa uzalishaji ulikuwa ni wajuu sana.
“Hata kama tumezalisha chakula kingi kuliko uwezo wetu wa maghala ya kutunza ,Watafiti wetu pia wanatakiwa kuja nawaje na  teknolojia nyepesi,rahisi na rafiki kwa makundi mbalimbali kwa jamii kuhakikisha kwamba mazao haya ambayo yamezalishwa kwa wingi hayapotei kwasababu tu hatuna teknolojia nzuri”,aliongeza Rukonge.
Hata hivyo Mkutano huoujadili fursa mbalimbali zilizopo katika mabadiliko ya Tabia ya nchi ambapo fursa zenyewe ni kama uvunaji wa maji,kuwekeza kwenye Teknolojia ya     Uzalishaji wa mbegu na Teknolojia ya Utunzaji wa Mazao.
Mkutano huo ni wa siku mbili unatarajia kufanyika Jijini Dodoma wiki ijayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527