Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Foundation kwa kushirikiana na Wentworth Africa Foundation imekabidhi Taulo za kike 976 kwa Shule ya Wasichana Ilulu iliyopo Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi. Tukio hilo la kukabidhi Taulo kwa wanafunzi limefanyika Novemba 21,2019 shuleni hapo mbele ya Mkuu wa Shule ya Wasichana Ilulu Bi. Amina Said Mandai kutoka kwa Katibu Msaidizi wa Taasisi ya WAMA Bw. Said Juma ambaye amemuwakilisha Mwenyekiti wa WAMA Mhe. Salma Kikwete, Mjumbe wa Bodi ya Wentworth Bi.Sauda Kilomanga na Mkurugenzi wa Wentworth Africa Foundation Bi. Anna Ndikumwani.
Kutoka kushoto ni Bi. Amina Said Mandai Mkuu wa Shule ya Wasichana Ilulu, Mjumbe wa Bodi ya Wentworth Africa Foundation Bi. Sauda Simba Kilomanga, Mkurugenzi wa Wentworth Bi. Anna Ndikumwani na Katibu Msaidizi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Foundation Bwana Said Hassan Juma
Social Plugin