VIJANA CHADEMA WAMCHUKULIA FOMU MBOWE ILI AGOMBEE TENA UENYEKITI CHADEMA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, November 25, 2019

VIJANA CHADEMA WAMCHUKULIA FOMU MBOWE ILI AGOMBEE TENA UENYEKITI CHADEMA

  Malunde       Monday, November 25, 2019

Vijana ambao ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamemchukulia fomu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Alikaeli Mbowe, ili kumshawishi agombee uenyekiti wa chama hicho na kuendelea kutetea kiti chake.

Tukio hilo limetokea leo Novemba 25, 2019 katika Ofisi za Chadema, Wilayani Kinondoni, Dar es Salaam,  baada ya vijana hao kuchukua fomu.

Chama hicho kitafanya uchaguzi wa viongozi Desemba 18, 2019 ambapo shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu itahitimishwa Novemba 30, 2019.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo, Daniel Ngogo,  aliyeratibu zoezi hilo, amesema wamefanya hivyo wakiamini kwamba, Mbowe atawavusha salama katika siasa za sasa.

Naftali ameeleza kuwa zaidi ya watu elfu ishirini na nane (28000) wamesaini petition ya kuitikia wito wakumuomba mwenyekiti wa CHADEMA kuridhia kuendelea kukiongoza chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano inayoishia Nov 2024.

“Tumechangisha fedha kwa watu wa kawaida. Mpaka jana tumepata Mil 5.6. Tunatambua fomu ni Sh. 1 milioni, lakini tulikuwa hatuna mfumo wa kuzuia watu kuchangia.

“Tumeshalipia fomu. Itakayobaki tunamkabidhi mwenyewe,” amesema Ngogo akiongeza kwamba watamkabidhi Mbowe fomu hiyo, siku ya Jumatano, Novemba 27, mwaka huu.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post