CUF NAO WACHOMOA BETRI..WATANGAZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba amesema Chama chake hakitoshiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na hakiutambui uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Mwezi huu mwishoni kwa madai ya ukiukwaji wa Haki na Sheria katika mchakato wake.

Profesa Lipumba ametoa msimamo huo leo Jumanne Novemba 12, 2019 wakati akitoa maazimio ya kikao cha baraza kuu la uongozi la CUF.

CUF kinakuwa chama cha siasa cha sita kujitoa katika uchaguzi huo baada ya Chadema, ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi, UPDP na Chauma.

Katika maelezo yake Profesa Lipumba amesema baraza hilo limetafakari kwa kina na kuona hakuna umuhimu kushiriki uchaguzi baada ya hoja zao tatu walizoziwasilisha serikalini kutofanyiwa kazi.

Profesa Lipumba amewataka asilimia nne ya wagombea wa chama hicho waliopitishwa kugombea kujitoa na kuiomba Tamisemi kutotumia nembo ya chama hicho kwenye uchaguzi huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527