SUMAYE APIGWA CHINI UCHAGUZI CHADEMA


Aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye ameshindwa kutetea nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura ya hapana.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Alhamisi Novemba 28, 2019 mjini Kibaha Mkoa wa Pwani, Sumaye aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mwaka 1995 hadi 2005 amepigiwa kura 28 za ndio na 48 za hapana na kura moja imeharibika.

Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Patrick Ole Sosopi ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

Akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo, Sumaye amesema lililofanyika ni demokrasia japo hana uhakika kama kutoa adhabu kwa mtu aliyekuwa anatumia haki yake kufanya demokrasia ni sahihi.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo baadhi ya wajumbe na wanachama waliokuwepo walilipuka kwa shangwe huku wakiimba nyimbo mbalimbali za chama.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post