Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwanamke aitwaye Pendo Nena (20) mkazi wa kijiji cha Mwanima, kata ya Busangwa wilaya ya Kishapu na mkoa wa Shinyanga ameuawa kwa kunyongwa na kuvunjwa shingo na mmewe John Paulo (27) kutokana na wivu wa mapenzi.
Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Novemba 3,2019 majira ya saa tatu asubuhi ambapo mwanamke huyo aliuawa kwa kunyongwa shingo yake ndani ya chumba chao cha kulala.
“Baada ya kufanya mauaji hayo John Paulo alikwenda katika kijiji cha Mwakolomwa na kujinyonga juu ya mti kwa kutumia kamba ya chandarua.
Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi. Mbinu iliyotumika ni kumnyonga shingo na kuivunja”,amesema Kamanda Abwao.
Kamanda Abwao anatoa wito kwa wananchi kufuata Sheria za nchi, sambamba na kuomba ushirikiano wa viongozi wa dini katika kuelimisha jamii.
Social Plugin