SERIKALI YARIDHISHWA NA UBORA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA ILEMELA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI), Dkt. Dorothy Gwajima amekagua ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya Ilemela mkoani Mwanza na kuridhishwa na ubora wa miundombinu ya majengo katika Hospitali hiyo. 

Dkt. Gwajima alifanya ziara ya kukagua ujenzi huo Novemba 07, 2019 na kisha kuelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuanza taratibu za kuhakikisha Hospitali hiyo inaanza kutoa huduma kuanzia mwaka ujao 2020 ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi. 

Naye Msanifu Majengo Mwandamizi OR- TAMISEMI, Jonaphry Rwabagabo alitoa rai kwa wahandisi katika Halmashauri nyingine 67 nchini zinazojenga Hospitali za Wilaya kutimiza vyema majukumu yao ili kuhakikisha wanatekeleza kwa ubora miradi hiyo kama ilivyoonekana katika majengo ya Hospitali ya Wilaya Ilemela. 

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela ulianza mwezi Machi 2019 kwa kutumia mfumo wa "Force Account" ambapo Serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza
Majengo mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya Ilemela inayojengwa katika Kata ya Sangabuye (eneo la Kabusungu-Isanzu).
 Mwonekano wa majengo mbalimbali.
 Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela uko katika hatua za mwisho ambazo ni pamoja na kuweka milango pamoja na madirisha.
 Ukaguzi ukiendelea katika Hospitali ya Wilaya Ilemela.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI), Dkt. Dorothy Gwajima akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa huduma za afya mkoani Mwanza.
Tazama Video hapa chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527