HUKUMU YA RAIS WA ZAMANI WA TFF JAMAL MALINZI NA WENZAKE KUSOMWA DISEMBA 5 MWAKA HUU | MALUNDE 1 BLOG

Friday, November 22, 2019

HUKUMU YA RAIS WA ZAMANI WA TFF JAMAL MALINZI NA WENZAKE KUSOMWA DISEMBA 5 MWAKA HUU

  Malunde       Friday, November 22, 2019

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itatoa hukumu dhidi ya Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi na wenzake watatu Desemba 05 mwaka huu.


Malinzi, Mwesigwa, Mwanga na Flora wanakabiliwa mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha Dola za Kimarekani 173,335.

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa jana lakini Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, alisema bado haijakamilika na kwamba itasomwa tarehe iliyopangwa.

Kesi hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Maira Kasonde lakini kwa sasa amehamishwa kituo cha kazi

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kusikiliza hukumu na upande wa Jamhuri ulikuwa tayari.

Hata hivyo, Hakimu Shaidi alisema hukumu ya kesi hiyo itasomwa Desemba 5, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post