GARI LA COASTAL UNION LIKIWA NA MASHABIKI WALIOENDA KUMSHANGILIA BONDIA MWAKINYO LAPATA AJALI

Gari la Coastal Union iliyokuwa imebeba mashabiki kutoka Tanga ambao walienda Dar kumuunga mkono Bondia Mwakinyo limepata Ajali kwa kugongana na lori maeneo ya Bunju ikitokea Dar kurudi Tanga. 


Kwa Mujibu wa Mganga Mkuu Bagamoyo,Dkt Azizi Msuya, majeruhi walikuwa zaidi ya kumi na sita lakini kumi ndio walikuwa na hali mbaya, kati ya hao wawili wamefariki, sita wamepata huduma ya kwanza na wameomba wakatibiwe zaidi Bombo, wawili wamepata rufaa kwenda Muhimbili, na wengine wanaendelea vizuri


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527