CHAMA TAWALA SUDAN CHAFUTWA

Sheria imepitishwa nchini Sudan ya kuvunja chama cha rais aliyeng'olewa madarakani Omar al-Bashir.

Bwana Bashir alichukua mamlaka 1989 kwa mapinduzi na kuliongoza taifa hilo kwa takriban miongo mitatu, hadi alipoondolewa kwa vuguvugu la maandamano ya upinzani mwezi Aprili.

Mamlaka inayoongoza kipindi cha mpito nchini humo pia imeondoa sheria ya umma ambayo ilitumiwa kudhibiti mienendo ya wanawake.

Hatua zote zimejibu madai muhimu ya vuguvugu la waandamanaji, ambayo yalilenga kuvunja utawala wa rais Bashir.

Sudan kwa sasa inaongozwa na utawala uaojumuisha jeshi na baraza la kiraia pamoja na baraza mawaziri la raia linaloongozwa na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok.

Hii ina maana gani?

Kuvunjwa kwa chama tawala cha Bwana Bashir cha National Congress Party (NCP) inamaanisha kuwa mamlaka zinaweza kuhodhi mali za chama .Sheria imethibitisha kuwa kamati itaundwa kutekeleza hili.

Hii inafanyika ili'' waweze kurejesha utajiri ulioibiwa wa watu wa Sudan ". alisema Bwana Hamdo katika ujumbe wake wa Twitter.

Sheria hiyo pia inasema "hakuna nembo yoyote ya utawala au chama itakayoruhusiwa kuhusika katika shughuli yoyote ya kisiasa kwa miaka 10 ''

Msemaji wa Muungano wa wasomi wa Sudan, kikundi cha waandamanaji kilichompindua rais al-Bashir, ameiambia BBC kuwa huu ulikuwa ni " wakati wa kihistoria".

"Huu ni wakati wa ahueni , kwasababu kila mtu nchini Sudan ameathiriwa vibaya kwa namna moja au nyingine na utawala ," alisema msemaji Samahir Mubarak.

Hata hivyo mchambuzi wa siasa kikanda na Bwana Mohammed Issa, anasema inapotokea hali kama iliyoikumba Sudan kama yaliyotokea sudan ambapo chama tawala kilichokuwa madarakani kinapinduliwa hatua ya kukivunja chama tawala haina maslahi kwa mustakabal wa Sudan.

''Hatua iliyochukuliwa na viongozi wa mpito kujenga utengamano haina maslahi katika kujenga utengamano wa Wasudan. Ilitarajiwa kwamba kungekuwa na ujumuishaji wa makundi yote katika siasa za nchi kwa ajili ya mustakbal.'', ameiambia BBC Bwana Issa kutoka Dar es salaam Tanzania.

Anasema:''kuvunjwa kwa chama cha National Congress (NCP), kinawaacha viongozi na wafuasi wa chama kile na washirika kama vile wafuasi wa kundi la Janjaweed bila uwanja wa kuelezea maoni yao ya kisiasa, na hali hiyo inaweza kuwafanya waelezee hisia zao kwa njia ya vita na uasi''.

Ni sheria gani nyingine zilizobadilishwa?

Sheria tata za umma ambazo zilikiuka vibaya haki za wanawake pia ziliondolewa.

Wanaharakati wanasema chini ya sheria za ukandamizaji, zenye misingi ya ufafanuzi sheria ya Kiisalmu (Sharia) , wanawake walikamatwa kwa kuhuduria mikutano ya binafsi ya chama au kwa kuvaa suluari.

Wahaharakati wa haki za binadamu wanasema maelfu ya wanawake walikamatwa na kupigwa kwa mienendo isiyofaa kila mwaka, na sheria zilitumiwa kiholela.Mabadiliko yaliyotangazwa na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok yalitimiza madai muhimu ya waandamanaji

Wairi Mkuu Hamdok alituma ujumbe wa Twitte : " Sheria za umma pamoja na maadili ya umma zilitumiwa kama chombo cha unyonyaji, kuaibisha na ukiukaji wa haki za raia na ukiukaji wa hadhi ya watu.

"Ninatuma ujumbe heshima kwa vijana wa kike na kiume wa nchi yangu ambao wamepitia masaibu ya utekelezwaji wa sheria hizi."

Tarehe 25 Novemba, Sudan ilifanya matembezi ya kwanza ya maadhimisho ya miongo kwa ajili ya Siku ya kimataifa ya kutokomeza ghasia dhidi ya wanawake.

Wanawake walikua mstari wa mbelekatika vuguvugu lililomg'oa madarakani Bwana Bashir.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post