Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ameendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo katika jimbo hilo ambapo Novemba 23, 2019 ametoa ahadi ya mbao 700 zenye thamani ya shilingi milioni 4.2 kwa ajili ya upauaji wa Zahanati ya Kijiji cha Imalanguza.
Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara huku pia akitoa ahadi nyingine ya mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Imalanguza.
Na George Binagi-GB Pazzo, Geita
Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano huo.
Wakazi wa Kata ya Bukombe wakimsikiliza mbunge Doto Biteko kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Imalanguza.
Mwonekano wa Zahanati ya Imalanguza ambayo pia mbunge Doto Biteko amekabidhi mabati 250 kwa ajili ya upauaji.
Diwani wa Kata ya Bukombe, Rozalia Masokola akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
Tazama Video hapa chini