WAZIRI WA NISHATI ASIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA MITAMBO WA KITUO CHA KUPOOZA UMEME CHA UBUNGO | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, October 3, 2019

WAZIRI WA NISHATI ASIMAMISHA KAZI MSIMAMIZI WA MITAMBO WA KITUO CHA KUPOOZA UMEME CHA UBUNGO

  Malunde       Thursday, October 3, 2019

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani amemsimamisha kazi Msimamizi wa Mitambo wa Kituo cha kupooza Umeme cha Ubungo Samson Mwangalume, kwa uzembe uliosababisha kukatika umeme jana usiku Oktoba 2, 2019, karibu Jiji zima la Dar es Salaam  huku chanzo kikielezwa kuwa ni uchafu wa vikombe katika njia za kusafirisha nishati hiyo.
Dk Kalemani pia ametoa onyo la mwisho kwa kaimu meneja mwandamizi wa usafirishaji wa umeme, Amos Kahiyula kuhakikisha haukatiki kutokana na uzembe.

Ametoa maagizo mara baada ya kutembelea kituo hicho na kutoridhishwa na maelezo ya Kahiyula aliyetoa sababu hizo baada ya kutakiwa na waziri huyo kueleza chanzo.

"Nataka huyo Samson aliyekuwa mkuu wa zamu asimamishwe kazi kuanzia leo na maelezo yake niyapate leo ofisini kwangu  kwani kama ni vikombe vipo kwa nini hamkuviweka,” amesema Dk Kalemani.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post