WAGANGA WA KIENYEJI WAONYWA KUWAPA TIBA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 22, 2019

WAGANGA WA KIENYEJI WAONYWA KUWAPA TIBA WATOTO WENYE VICHWA VIKUBWA

  TANGA RAHA BLOG       Tuesday, October 22, 2019

 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga leo kulia ni Mjumbe wa Chama hicho Taifa Oscar Changala
 OFISA Habari wa Mkoa wa Tanga Zuberi akichangia jambo kwenye mkutano huo

 SEHEMU ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania 
 MWENYEKITI wa Klabu ya Waaandishi wa Habari Mkoani Tanga Hassan Hashim akichangia jambo kwenye mkutano huo
Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph akiuliza swali kwenye mkutano huo
WAGANGA wa Kienyeji hapa nchini wametakiwa kuacha kuwapokea na kuwapa tiba watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi badala yake wawahimiza wazazi kuwapeleka hospitalini kupatiwa matibabu ili kuondosha tatizo hilo.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazazi chenye malengo ya kutoa elimu ya Kichwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) Abdulhakim Bayakub wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Alisema kumezuka tabia ya baadhi ya waganga wa kienyeji kuwapokea wagonjwa hao huku wakijua kwamba hawawezi kuwatibu matatizo waliyonayo jambo ambalo limepelekea asilimia kubwa wengi wao kuzidiwa na ugonjwa walionao.

“Ndugu zangu waganga wa kienyeji acheni kuwapokea na kuwapa tiba watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi badala yake wazazi wahakikishe mnawapaleka kuwapeleka hospitalini kupatiwa matibabu ili kuondosha tatizo hilo”Alisema.

“Lakini pia acheni kusema kwamba watoto wenu wamerogwa, balaa wala mikosi bali wapelekeni hospitalini wapate tiba ya magonjwa yanayowakabili “Alisema

Hata hivyo aliwataka pia wasiende kwenye maombi,makanisani wale misikitini badala yake waende hospitalini kwenda kupatiwa matibabu ambayo yatawasaidia kuondokana na matatizo yanayowakabili.

“Wananchi achaneni na imani potofu juu ya ugonjwa huo huku akitaka waupige vita kwani baadhi yao wana imani kuwa ni mizimu jambo ambalo halina ukweli wowote.

Awali akizungumza katika mkutano huo Afisa Ustawi wa Jamii Mmasa Malugu aliwataka waandishi wa habari kutumia vema kalamu zao ili kuweza kusaidia kuwafichukua watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi waliopo kwenye jamii.

Alisema kwamba lazima jamii ibadilike na kuondokana na fikra potovu kuhusiana na kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala yake wawapeleke hospitali ili waweze kupatiwa matibabu.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post