MKANDARASI AVUNJA MADIRISHA YA ALUMINIUM BAADA YA HALMASHAURI 'KUZINGUA' KUMLIPA PESA ZAKE | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, October 8, 2019

MKANDARASI AVUNJA MADIRISHA YA ALUMINIUM BAADA YA HALMASHAURI 'KUZINGUA' KUMLIPA PESA ZAKE

  Malunde       Tuesday, October 8, 2019

Mkandarasi aliyefahamika kwa jina la  Boniface Exavery, ambaye alitengeneza madirisha ya Almunium na katika Kituo cha Afya cha Katumba, Halmashauri ya Nsimbo ya mkoani Katavi, ameyavunja madirisha hayo, kwa kile alichokidai kutokamilishiwa malipo yake na ofisi ya Halmashauri huku akiwaameshamaliza kazi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, amedai mradi huo ulikuwa umekiuka taratibu mbalimbali za kisheria, ikiwemo upatikanaji wa tenda hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, mwenyewe ameeleza kushtushwa na hatua ya Mkandarasi huyo, na kueleza taarifa za awali walizipata kutoka kwa wananchi, na kulitaka Jeshi la Polisi kumshikiria Mkandarasi huyo, huku akikiri Halmashauri kutomlipa malipo yake.

Mmoja wa Wakandarasi ambaye anajulikana kama Bulaya Mushi, ambaye na yeye anaidai Halmashauri hiyo kwenye mradi huo wa Kituo cha Afya, amemuomba Mkuu wa Mkoa kuangalia madai yao ili waweze kulipwa na Halmashauri hiyo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post