MHUBIRI AFUKUZWA RWANDA KWA KUENEZA INJILI FEKI.. 'KASEMA WANAWAKE IBILISI'

 Mhubiri mmoja kutoka Marekani amefurushwa nchini Rwanda kwa madai ya kueneza injili feki. 

Kulingana na gazeti la the New Times la Rwanda, Greg Schoop alipandishwa ndege ya kurudi kwao Marekani Jumatatu, Oktoba 7,2019.

Hatua hiyo imejiri wakati ambapo redio ya mhubiri huyo ilifungwa na serikali nchini Rwanda baada ya kusema akina mama ni ibilisi. 
“Gregory Schoof Brian amerudishwa nchini mwao kama mhamiaji aliyepigwa marufuku," gazeti hilo lilimnukuu afisa wa uhamiaji Regis Gatarayiha.

 Redio hiyo kwa jina Amazing Grace ilikuwa imepeperusha matangazo ya mhubiri Nicolas Niyibikora yaliyoleta utata mkubwa. "Wanawake walio kati yetu ni malaya.

 Akina mama walileta dhambi duniani na ikiisha ni kwa sababu ya wanawake," mhubiri huyo alidaiwa kusema.


Duru ziliarifu kuwa mhubiri huyo alikuwa amekamatwa hapo awali na kutakiwa kuomba msamaha kuhusu matamshi yaliyofanywa kwenye redio yake lakini akakataa.

 Kando na injili yake iliyomchafua mwanamke katika macho ya umma, Greg pia inaarifiwa alikuwa ameikosoa serikali ya Rais Paul Kagame na kusema kuwa iko katika safari ya kupeleka wananchi jehanamu.

Serikali ya Rais Paul Kagame imekuwa ikikabiliana na wahubiri wanaodaiwa kueneza injili feki nchini humo. 

Tayari, zaidi ya kanisa 700 zimefungwa nchini humo pamoja na wahubiri wote kutakiwa wawe na shahada katika masuala ya theolojia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527