UTIAJI SAINI MKATABA WA UKARABATI MKUBWA WA UJENZI WA JUMBA LA BAITUL EL AJAIB WAFANYIKA ZANZIBAR | MALUNDE 1 BLOG

Friday, October 11, 2019

UTIAJI SAINI MKATABA WA UKARABATI MKUBWA WA UJENZI WA JUMBA LA BAITUL EL AJAIB WAFANYIKA ZANZIBAR

  Malunde       Friday, October 11, 2019
Na Miza Kona Maelezo 11/10/2019

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Oman imetiliana saini mkataba wa Ukarabati wa ujenzi Jengo la Urithi wa Mji Mkongwe Beit el -Jaibu.

Hafla hiyo ya utiaji saini imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale baina ya katibu Mkuu wa wizara hiyo Bi Khadija Bakar Juma na Katibu Mkuu wa Mambo ya Urithi na Utamaduni wa Serikali ya Oman Bwana Salim Mohammed Mahrouk.

Akizungumza katika Utiaji saini huo Waziri wa Habari na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo amesema Zanzibar ni nchi ya 10 katika nchi zenye Miji ya Urithi wa dunia hivyo imeamua kulifanyia ukarabati jengo hilo ili lisiondoke katika nchi zenye urithi huo na kuongeza hadhi ya miji yenye vivutio vya uasili.

Amesema kuwa jengo hilo litakarabatiwa bila ya kubadilishwa na kuondosha uhalisia wake wa zamani  ili liweze kudumu kwa muda mrefu na urithi mzuri wa vizazi vijavyo na kuwa vivutio kwa watalii.

Waziri Mahamoud amefahamisha serikali itayafanyia ukarabati majengo ya kihistoria yaliyochakaa na kuyarejesha katika hali yake ya zamani ili kuongeza hadhi ya miji yenye historia na vivutio kwa wageni.

Ameeleza kuwa serikali ya Oman imekuwa ikisaidia Zanzibar katika Nyanja mbali mbali kwa lengo la kuleta maendeleo na kudumisha mashikiano makubwa yalipo.

Nae katibu Mkuu wa Mambo Urithi na Utamaduni wa Oman Bwana Salim Mohammed Mahrouk amesema serikali ya Oman itaendelea kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha Utamaduni na Urithi na kuleta maendeleo zaidi

Mapema Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Mji Mkongwe Issa Sarboko Makarani amesema watahakikisha kuwa jengo la Beit-el Jaibu linakwenda sambamba kushajihisha wananchi kuyafanyia ukarabati majengo yao yaliyomo mji mkongwe  

Ujenzi huo ni wa miaka miwili ambao unaokarabatiwa na kampuni ya Gilardi kutoka Itali ambao utagharimu jumla ya sh bilioni 14 hadi kumalizika kwake.   


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post