MWANAMKE AJIUA KWA KANGA KISA AMEAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI

Picha ya Kanga,haihusiani na habari hapa chini


Na Walter Mguluchuma - Malunde 1 blog Nkasi
Mwanamke aliyefahamikakwa jina la Shija Lutonja (23) mkazi wa kijiji cha Kakoma wilayani Nkasi mkoani Rukwa amejinyonga kwa kutumia kanga yake huku akiacha ujumbe kuwa amepata maambuzi ya Virusi vya UKIMWI na mmewe yupo kafungwa jela.

Akizungumza na Malunde1 blog, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kakoma Richard Kandege amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya kati ya saa tatu hadi nne asubuhi ambapo mwanamke huyo alikutwa amejinyonga nje ya mji wake kwenye mti kwa kutumia kanga.

"Aligundulika amejinyonga baada ya watu waliokuwa wakipita katika maeneo hayo kuona mwili ukining’inia juu ya mti na kutoa taarifa haraka kwenye ofisi ya serikali ya kijiji kisha tulitoa taarifa polisi",ameeleza.


"Polisi walifika eneo la tukio na katika uchunguzi wao hawakuona majeraha yoyote katika mwili wa marehemu zaidi ya yale ya kujinyonga. Walikuta ujumbe mfupi wa maneno kwenye mwili wa marehemu aliouandika kuwa ameamua kujiua mwenyewe kwa sababu ya kuwa amepimwa na amekutwa na Virusi vya Ukimwi lakini pia mumewe amefungwa jela hivi karibuni hivyo haoni sababu ya yeye kuendelea kuishi hapa duniani",amesema Kandege.


Mwenyekiti huyo wa kijiji amesema tukio hilo limeacha simanzi kubwa katika kijiji hicho kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa Mwanamke katika kijiji hicho kuchukua maamuzi kama hayo ya kujinyonga hadi kufa.

Mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuitaka jamii kuacha kujichukulia sheria mikononi wakati jambo lake lilikuwa ni la kawaida kabisa kwani si yeye mtu pekee katika wilaya hiyo mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi bali alipaswa kuwashirikisha watu anao waanini ili wamempe ushauri na asingefikia hatua hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527