POLISI ARUSHA WAWATAKA WANANCHI KUTUMIA SIKU 3 ZA NYONGEZA WAJIANDIKISHE DAFTARI LA WAPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, October 13, 2019

POLISI ARUSHA WAWATAKA WANANCHI KUTUMIA SIKU 3 ZA NYONGEZA WAJIANDIKISHE DAFTARI LA WAPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

  Malunde       Sunday, October 13, 2019

Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewaondoa wasiwasi wakazi wa jiji la Arusha na kuwataka wajitokeze kwa wingi kuijiandikisha katika daftari la wapiga kura la uchaguzi mdogo wa serikali za mtaa katika siku tatu ambazo serikali imeongeza hadi kufikia tarehe 17 octoba mwaka huu kwani jeshi hilo limeimarisha ulinzi na usalama wa kutosha kwa wananchi wote.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana amesema kuwa kufutia serikali kuongeza siku za kujiandikisha jukumu lao ni kuhakikisha usalama kwa wananchi wote kwani jeshi litafanya kazi bila kupendelea chama chochote cha siasa.

Kamanda Shana amesema serikali inawajali wananchi wake na kuamua kuwaongezea siku za kujiandikisha ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Kamanda huyo amesema kuwa jeshi hilo linafanya kazi kwa kuzingatia kanuni,taratibu na miongozo mbalimbali katika kutekeleza wajibu wake wa msingi.

“Tunawaomba wakazi wa Arusha wajitokeze kwa wingi katika siku hizi zilizoongewa wajiandikishe kwa wingi na pia wajitokeze kupiga kura” Alisema Kamanda
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post