MAKONDA AAGIZA MADUKA YOTE DAR KESHO YAFUNGULIWE SAA 5 ASUBUHI ILI KUTOA NAFASI KWA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Paul Makonda amesema, siku ya kesho maduka yote mkoani humo yatafunguliwa kuanzia saa 5 asubuhi ili kupisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuenzi miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa


Makonda ametoa agizo hilo leo Jumapili Oktoba 13, 2019 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

RC Makonda amesema kwakuwa kesho ni Siku ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameona ni vyema Wananchi wote wakamuenzi Baba wa Taifa kwa kuhakikisha wanapata Nafasi ya Kutosha ya Kujiandikisha ili waweze kuchagua Viongozi wa mitaa wanaoweza kutatua matatizo yao.

Aidha RC Makonda amewasihi Wamachinga, Bodaboda, Makondakta, madereva, Viongozi wa Taasisi, wafanyakazi wa Bar, Saloon, wamiliki na wafanyakazi wa Sehemu za Starehe kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa, Shule za Msingi,  sekondari na sehemu zilizowekwa mahema maalumu ya kujiandikisha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527