WANANCHI WASHAURIWA KUJIEPUSHA NA VICHOCHEO VYA MARADHI YA MOYO | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, October 5, 2019

WANANCHI WASHAURIWA KUJIEPUSHA NA VICHOCHEO VYA MARADHI YA MOYO

  Malunde       Saturday, October 5, 2019
Wananchiwametakiwa kupunguza utumiaji wa vileo, uvutaji wa sigara pamoja na vyakula vyenye mafuta mengi ikiwemo chapati, mandazi na vitumbua kwani vinavyochochea ongezeko la maradhi ya moyo na badala yake wamehimizwa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara.

Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Maradhi ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando iliyopo jijini Mwanza, Prof. William Mahalu ametoa rai hiyo Oktoba 05, 2019 kwenye mazoezi/matembezi ya afya yaliyofanywa na wafanyakazi wa hospitali hiyo ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho kilele ya Siku ya Moyo Duniani 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakiwa kwenye mazoezi ya afya katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wakihitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani 2019 kwa kufanya mazoezi ya afya.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando wameweka utaratibu wa kufanya mazoezi ya afya mara mbili kila mwezi ili kutoa hamasa kwa wananchi wengine kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi.
Matembezi/ mazoezi ya afya kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Rifaa ya Kanda ya Ziwa Bugando iliyopo jijini Mwanza.
Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani hufanyika kila mwaka Septemba 29.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani 2019 ni "ahadi ya moyo wangu, moyo wako na mioyo yetu sote" ikilenga kuhamasisha kila mmoja katika jamii kuwa balozi wa kuzingatia kanuni za kiafya ikiwemo mazoezi na ulaji wa vyakula ili kuepukana na maradhi ya moyo.
Mratbi wa Mazoezi kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa Bugando akisisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi.
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Prof. William Mahalu (kushoto) akizungumza baada ya mazoezi/ matembezi hayo kufikia tamati.
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Prof. William Mahalu (katikati) akizungumza na wanahabari.
Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando, Prof. William Mahalu (kulia) akionesha baadhi ya nembo za wafadhili waliosaidia upatikanaji wa tisheti kwa ajili ya matembezi hayo.
Tazama Video hapa chini

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post