MFANYABIASHA YUSUFU ALLY MAARUFU KWA JINA LA 'MPEMBA WA MAGUFULI' AANDIKA BARUA KWA DPP KUKIRI MAKOSA YAKE | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, October 10, 2019

MFANYABIASHA YUSUFU ALLY MAARUFU KWA JINA LA 'MPEMBA WA MAGUFULI' AANDIKA BARUA KWA DPP KUKIRI MAKOSA YAKE

  Malunde       Thursday, October 10, 2019

Mfanyabiashara Yusufu Ally, maarufu kwa jina la mpemba wa Magufuli na wenzake,wanaokabiliwa na mashitaka ya  uhujumu uchumi ikiwemo kujihusisha na biashara ya meno ya tembo, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuomba kukiri mashitaka yao hayo.


Katika kesi hiyo, mbali ya Mpemba washitakiwa wengine ni Charles Mrutu, Benedict Kungwa, Jumanne Chima, Ahmed Nyagongo na Pius Kulagwa.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde amemueleza dai Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba washitakiwa wameshaandika barua hivyo, anaomba mahakama iwape muda kwa ajili ya kuingia katika makubaliano.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 16, mwaka huu 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa hao  wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6 .

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo 50 vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh  milioni 392.8  bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Pia inadaiwa Oktoba 26, mwaka huu, washitakiwa hao wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande vya meno ya tembo10 vyenye   uzito wa kilo 13.85 vya thamani ya Dola za Marekani 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.

Wanadaiwa kuwa  Oktoba 27, mwaka huu, wakiwa Tabata Kisukuru washitakiwa hao walikutwa na vipande vinne vya meno hayo ya tembo yenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya Dola za Marekani 15,000  sawa na Sh milioni 32.7 .

Pia, Oktoba 29, mwaka huu walikutwa na vipande 36 vya thamani ya Sh  milioni 294.6   bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post