MEYA WA JOHANNESBURG AJIUZULU | MALUNDE 1 BLOG

Monday, October 21, 2019

MEYA WA JOHANNESBURG AJIUZULU

  Malunde       Monday, October 21, 2019
Herman Mashaba amekuwa Meya wa Johannesburg kwa miaka mitatu
Mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu wa kisiasa kutoka katika chama ambacho kihistoria kulikuwa ni cha wazungu walio wengi cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance (DA) amejiuzulu wadhfa wake kutokana na namna kinavyoshughulikia suala la asili za rangi za watu.

Herman Masaba alikuwa ni Meya wa Johannesburg kwa muda wa miaka mitatu.

Uchaguzi wa Meya mweusi kutoka katika chama cha DA ulionekana kama ishara ya ya kwamba chama hicho kinaweza kuwa tisho kwa chama tawala cha ANC na huenda kuchukua mamlaka ya taifa.

Lakini katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu Bwana Masaba amesema:

"Siwezi kuungana na watu ambao wanaamini kuwa asili ya rangi ya mtu sio muhimu katika mazungumzo yao kuhusu ukosefu wa usawa ."

Amesema kuwa uamuzi wake ulichochewa na kusajiliwa tena kwa Heln Zile, mwanasiasa mzungu ambaye alichochea hasira mwaka 2017 wakati aliposhabukia ukoloni katika ngazi ya juu ya vyeo katka chama hicho :

"Uchaguzi wa [Helen] Zille kama mwenyekiti wa baraza kuu ni ushindi kwa watu ambao wanapinga mfumo wangu wa imani .Mmusi Maimane (kushoto) alimrithi Helen Zille (kulia) kama kiongozi wa DA mnamo mwaka 2015

Viongozi weusi katika chama cha DA wanaoamini juu ya kuwepo kwa uhuru , chama chenye asili tofauti za watu kinarejea katika mizizi yake ya kuwa taasisi yenye wazungu pekee, anasema mwandishi wa BBC mjini Johannesburg Milton Nkosi.

Bwana Mashaba pia amesema kuwa "agenda inayowaunga mkono maskini " ya serikali "imepuuzwa, kukosolewa na kutajwa kuwa haiwezekani " na chama cha DA. Mwandishi wetu anasema kuwa hiyo "kuwaunga mkono maskini ", ina maanisha kuwa Bwana Mashaba "anawaunga mkono weusi".

Kama meya wa kwanza kuongoza mji mkubwa zaidi wa Afrika Kusini ambaye hakutoka chama tawala -ANC (African National Congress) tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu 1994, ushindi wa Bwana Mashaba mwaka 2016 uliashiria mafanikio makubwa kwa chama cha DA.

Akiwa ni mfanyabiashara aliyepata mafanikio binafsi Bwana Mashaba alionekana kama mshirika muhimu wa kiongozi wa kwanza wa chama hicho mweusi Mmusi Msimane, katika juhudi zake za kuongeza ufuasi miongoni mwa wapigakura weusi.

Hata hivyo kuraza DA zilipungua katika uchaguzi mkuu wa wa Mei baada ya mahafidhina wa kizungu kutelekeza chama hicho, na kurejea kwa Bi Zille katika wadhfa wa juu kunaonekana kama jaribio la kurejesha ufuasi wao.

Bwana Mashaba amesema kuwa atang'atuka madarakani mweiz ujao, huku maswali yakiibuka juu ya ikiwa DA itaweza kurejesha tena kiti cha umeya wa jiji la Johannesburg.
Ushindi wa Bwana Mashaba mwaka 2016 uliashiria mafanikio makubwa kwa chama cha DA

Mwandishi wa BBC Milton Nkosi anasema taarifa ya kujiuzulu kwa Herman Mashaba kumefichua uozo ndani ya chama cha DA ni mbaya kuliko ilivyokua wakati Mmusi Maimane alipochaguliwa kama kiongozi wa chama ambapo waliimba kuwa mikono yake iliofungwa na Helen Zille kama walivyokuwa wakiimba kwa sauti wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho.

Kwa serikali ya ANC, ambayo inaonekana imekwama katika mizozo ya ndani, matatizo hayo ndani ya chama cha upinzani cha DA ni baraka ya manna kutoka mbinguni.

ANC ni dhaifu lakini chama kukibwa zaidi cha upinzani nchini kinajigawanya chenyewe bila kuchokozwa.

Kwa kiongozi chama cha DA Bwana Maimane,pia napambana kwa ajili ya maisha yake ya kisiasa.

Akiwa bega kwa bega na Bwana Mashaba katika mkutano wa waandishi wa habari wa Jumatatu, Bwana Maimane alinyoosha mkono wake juu akisema : "Wewe ni shujaa wangu ! wewe ni shujaa wang !"

Hatma ya Bwana Maimane' itaamuliwa katika kongamano la mwaka ujao la chama . Lakini kulingana na kasi ya matukio yalivyo ndani ya chama, hakuna hakikisho kuwa ataendelea kuwa ndani ya chama wakati huo.
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post