MWANASHERIA TGNP MTANDAO : WANAWAKE MSIKUBALI KUTUMIA MIILI YENU KUWEZESHWA KISIASA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, October 23, 2019

MWANASHERIA TGNP MTANDAO : WANAWAKE MSIKUBALI KUTUMIA MIILI YENU KUWEZESHWA KISIASA

  Malunde       Wednesday, October 23, 2019

Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa Juma akizungumza kwenye mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Wanawake waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019 wametakiwa kulinda utu wao kwa kutokubali kutumia miili yao kuwezeshwa kisiasa kwani watapoteza uhalali mbele ya jamii. 

Ushauri huo umetolewa leo Jumatano Oktoba 23,2019 na Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa Juma wakati wa mafunzo ya uongozi kwa watia nia wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kutoka baadhi ya kata wilaya ya Kishapu kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa yaliyofanyika katika ukumbi wa BM Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. 

Juma ambaye ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo,alisema wanawake wanaowania nafasi za uongozi wa kisiasa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika kutafuta kuwezeshwa hali inayosababisha baadhi yao kujikuta wakitumia miili yao. 

"Tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,naomba muepuke rushwa ya ngono, wagombea wanawake msikubali kutumia miili yenu ili kuwezeshwa kisiasa",alisema Juma. 

"Mwanamke usiwe jamvi la wageni,usiwe daladala kila mtu anapanda,kila mmoja anapita je watapita wangapi?. Tumieni mbinu zingine siyo kutumia miili yenu,tambueni thamani yenu,utu wenu. Amini usiamini wengine watawatumia na hizo nafasi hamtazipata",alisisitiza.
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa Juma akizungumza wakati wa mafunzo ya uongozi kwa watia nia wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kutoka baadhi ya kata wilaya ya Kishapu kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa yaliyofanyika katika ukumbi wa BM Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga leo Jumatano Oktoba 23,2019. Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa Juma akizungumza wakati wa mafunzo ya uongozi kwa watia nia wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Sehemu ya wanawake watia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kutoka baadhi ya kata za wilaya ya Kishapu.

Soma pia : WANAWAKE WATIA NIA WAPEWA MAFUNZO KUGOMBEA NA KUSHINDA KWENYE UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post