DIWANI AHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MPIGA KURA


Diwani wa viti maalumu Manispaa ya Shinyanga Mhe. Mariam Nyangaka, ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura, ili siku ya uchaguzi wakafanye maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi bora ambao watawaletea maendeleo.

Nyangaka ametoa wito huo jana Oktoba 9,2019  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mtaa wa Kitangili Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga ukiwa na lengo la kusoma utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari hilo la mpiga kura , ili siku ya uchaguzi Novemba 24 mwaka huu wapate fursa ya kupiga kura na kuchagua viongozi makini, waadilifu, na watakaopigania maslahi ya wananchi katika kuwaletea maendeleo.

Pia ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi huo wa Serikali za mitaa, ili wapate kufikia usawa wa 50 kwa 50 kwenye uongozi, na kuacha kuogopa kushindana na wanaume ikiwa wanawake ni viongozi watendaji wazuri kuliko wanaume.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo wa Kitangili Habiba Jumanne, akisoma utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye mtaa wake, amesema ametegengeza barabara kilomita mbili za Changalawe, amefanikisha upimaji wa viwanja likiwamo eneo la soko, ametatua migogoro ya ardhi, pamoja na kujenga matundu ya vyoo na madawati kwenye shule ya msingi Kitangili.

Uandikishaji wa daftari la mtaa la mpiga kura umeanza Oktoba 8 na unatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 14 mwaka huu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Diwani wa viti Maalum Manispaa ya Shinyanga Mhe. Mariam Nyangaka akizungumza na wananchi wa Mtaa na Kata ya Kitangili mjini Shinyanga  na kuwataka wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura ili wapate fursa ya kupiga kura na kuchagua viongozi bora watakao waletea maendeleo. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Diwani wa viti maalum manispaa ya Shinyanga Mhe. Mariamu Nyangaka akizungumza na wananchi wa Mtaa na Kata ya Kitangili mjini Shinyanga  na kuwataka wanawake wajitokeze kuchukua fomu ya kugombea uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kitangili Habiba Jumanne akisoma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye mtaa huo.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Kitangili Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na kutakiwa wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Kitangili Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na kutakiwa wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Kitangili Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na kutakiwa wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mtaa la mpiga kura.

Mwananchi Zuhura Ramadhani wa Mtaa wa Kitangili akiuliza swali kwenye mkutano wa hadhara.

Mwananchi Jastine Thobias wa Mtaa wa Kitangili akiuliza swali kwenye mkutano wa hadhara.

Wananchi wa Mtaa wa Kitangili wakitawanyika baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara.

Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527