KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA MAPYA


Jeshi la Korea ya Kusini limesema, Korea Kaskazini imerusha makombora kutoka baharini hii leo. 

Kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini, huenda Korea kaskazini imefanya majaribio ya kombora la chini ya maji kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu kabla ya kuanza upya kwa mazungumzo ya nyuklia na Marekani mwishoni mwa wiki hii. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa jeshi wa Korea Kusini, Makombora hayo ya Korea Kaskazini yaliruka umbali wa kilometa 450 na urefu wa kilometa 910 usawa wa bahari kutoka eneo lisilojulikana kwenye bahari nje ya mji wa pwani wa Wonsan, Kaskazini Mashariki ya Korea kaskazini. 

Kwa mujibu wa msomi Du Hyeogn Cha, kutoka Taasisi ya Asan ya Mafunzo ya Sera ya mjini Seoul amesema Korea Kaskazini inajaribu kutoa ujumbe kwa Marekani kwamba inaweza kuchukua njia tofauti ikiwa mazungumzo hayatakwenda kama ilivyotaka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527