MBUNGE AZZA ATOA ZAWADI YA KOMPYUTA KUWAPA MOTISHA WALIMU SHULE YA SEKONDARI OLD SHINYANGA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, October 3, 2019

MBUNGE AZZA ATOA ZAWADI YA KOMPYUTA KUWAPA MOTISHA WALIMU SHULE YA SEKONDARI OLD SHINYANGA

  Malunde       Thursday, October 3, 2019
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa zawadi ya Kompyuta katika shule ya Sekondari Old Shinyanga ili kuwapa motisha walimu wa shule hiyo kutokana na kazi nzuri kuifanya shule hiyo kuwa na ufaulu mzuri kwenye mitihani.

Mhe. Azza ametoa zawadi ya Kompyuta kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya walimu leo Alhamis Oktoba 3,2019  wakati wa Mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika shuleni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta hiyo yenye thamani ya shilingi milioni mbili,Mhe. Azza alisema amefurahishwa jinsi shule hiyo ya kata inavyofanya vizuri kwenye mitihani mfano katika Matokeo ya Kidato cha sita mwaka 2019 imekuwa ya kwanza kati ya shule zote za mkoa wa Shinyanga.

"Nawapongeza sana walimu kwa kazi nzuri mnayofanya katika kuboresha elimu shuleni hapa.Naomba niwakabidhi Kompyuta hii kama motisha,naamini itawasaidia katika kazi mbalimbali za ofisi",alisema Azza.

Katika Mahafali hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko aliendesha harambee fupi kwa ajili ya kutatua upungufu wa viti na meza ambapo wazazi na wageni waalikwa walifanikisha kupatikana kwa vivi na meza 62 huku mbunge Azza akichangia shilingi laki moja na mkuu wa wilaya akiahidi kuchangia meza 50.

Mbunge huyo pi aliahidi kuwalipia ada wanafunzi wa kike watano watakaofaulu na kupata daraja la kwanza na la pili kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.

Jumla ya wanafunzi 120 kati yao wasichana 60 na wavulana wanahitimu elimu ya sekondari katika shule hiyo iliyopo katika wilaya ya Shinyanga.

Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi zawadi ya Kompyuta kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya walimu wa shule ya Sekondari Old Shinyanga.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi zawadi ya Kompyuta kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya walimu wa shule ya Sekondari Old Shinyanga.
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi zawadi ya Kompyuta kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko kwa ajili ya walimu wa shule ya Sekondari Old Shinyanga.
Makabidhiano yakiendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne shule ya Sekondari Old Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa mahafali ya kidato cha nne shule ya Sekondari Old Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akicheza muziki na wanafunzi wa shule ya Sekondari Old Shinyanga.
Wanafunzi wakisoma risala
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa ameshikilia kisu kwa ajili ya kukata keki wakati wa mahafali ya kidato cha nne shule ya sekondari Old Shinyanga.
Zoezi la kukata keki likiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko( kulia) na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad wakilishana keki


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post