MBUNGE AZZA HILAL ACHANGIA MASINKI YA VYOO SHULE YA MSINGI ILOLA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad amechangia masinki 11 ya vyoo ili kumaliza changamoto ya upungufu wa vyoo katika shule ya Msingi Ilola iliyopo katika kata ya Ilola halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mhe. Azza ametoa mchango huo Oktoba 2,2019 akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya Darasa la Saba 2019 katika shule ya Msingi Ilola ambapo jumla ya wanafunzi 75 wamehitimu elimu ya darasa la saba.

"Nawapongeza sana wananchi kwa kujitolea kujenga matundu 11 ya vyoo kwa nguvu zenu.Nimefurahi kuona ujenzi yamekamilika,ili kuunga mkono jitihada zilizofanywa na wananchi na mimi nachangia  masinki 11 ya vyoo ili kukamilisha ujenzi katika shule yetu ya Ilola.Tusiishie hapa naomba pia tuanzishe ujenzi wa vyoo kwa ajili ya walimu",alisema Azza.

Mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi wa wanafunzi waliohitimu elimu ya darasa la saba kutothubutu kuwaozesha wanafunzi hao.

"Wazazi na walezi msione kuwa watoto wamemaliza shule basi ndiyo muamue kuwaozesha,msijidanganye hawa bado ni wanafunzi  na wale ambao hawatafaulu msione kuwa ndiyo mwisho wa elimu, wasipofaulu kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza naomba muwapeleke kwenye vyuo vya ufundi badala ya kukimbilia kuwaozesha kwani hatutaki kuona mimba wala ndoa za utotoni",aliongeza Azza.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika kata ya Ilola halmashauri ya Shinyanga. Pichani masinki 11 ya vyoo yaliyotolewa na Mbunge huyo ili kumaliza changamoto ya upungufu wa vyoo katika shule hiyo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika kata ya Ilola halmashauri ya Shinyanga. Pichani masinki 11 ya vyoo yaliyotolewa na Mbunge huyo ili kumaliza changamoto ya upungufu wa vyoo katika shule hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akikabidhi masinki 11 ya vyoo kwa wajumbe wa kamati ya shule ya msingi Ilola.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akikabidhi masinki 11 ya vyoo ili kumaliza changamoto ya upungufu wa vyoo katika shule ya Msingi Ilola iliyopo katika kata ya Ilola halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi wakifuatilia matukio wakati wa mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Ilola
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akijiandaa kukata keki wakati wa mahafali ya shule ya Msingi Ilola iliyopo katika kata ya Ilola halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wazazi na walezi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Wanafunzi wakitoa burudani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527