JESHI LA POLISI DODOMA LAWANASA RAIA WANNE WA SOMALIA NA ETHIOPIA KWA UHAMIAJI HARAMU | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, October 24, 2019

JESHI LA POLISI DODOMA LAWANASA RAIA WANNE WA SOMALIA NA ETHIOPIA KWA UHAMIAJI HARAMU

  Malunde       Thursday, October 24, 2019
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma  linawashikilia Raia wanne kutoka nchini za Somalia na Ethiopia Kwa kuingia nchini bila kibali huku pia likiwashikilia watu wawili  Raia wa Tanzania waliokuwa wakiwasafirisha  wahamiaji haramu hao .

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Okt.24,2019  jijini Dodoma,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Girres Muroto amesema mnamo tarehe 23,10,2019  majira ya saa 10:00 huko katika kijiji na kata ya MTERA  Tarafa ya RUDI Wilaya ya MPWAPWA   Mkoani Dodoma ,walikamatwa wahamiaji haramu wanne walioingia nchini bila vibali.

Kati yao ,Wawili ni Raia wa Ethiopia  na Wawili ni Raia wa SOMALIA huku pia wakikamatwa watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha wahamiaji haramu hao kutoka ARUSHA Kwenda IRINGA kwa Kutumia Usafiri wa pikipiki mbili .

Waliokamatwa ni Sellamu Yohanes[24] Raia wa Ethiopia,Ashetu Tesfaye[20]Raia wa Ethiopia,Mahamoud Mapaa[19]Raia wa Somalia,Cuse  Ciise [18]Raia wa Somalia 

Kamanda Muroto amewataja Raia wa Kitanzania waliokuwa wakiwasafirisha wahamiaji haramu hao kwa kutumia pikipiki ni Jamali Babuu Martin [26] dereva wa bodaboda ,mkazi wa ORASITE ARUSHA akiendesha pikipiki  namba MC 942 AXK KINGLION Chassis Na.LTBPK8BG5F2KO9729 rangi nyeusi.

Mwingine ni Wiston Alex  MAKIA  ALLY [25] Dereva wa Bodaboda mkazi wa Mbauda ARUSHA akiendesha pikipiki Na.MC 767 CEB DAYUN  Chassis Na.L7GPCJLYH1099156 rangi nyeusi.

Kamanda Muroto ametaja mbinu waliyotumia kuingia nchini ni  kwa kutumia usafiri wa pikipiki kuvuka mipaka na vizuizi vya barabarani.

Aidha ,amebainisha kuwa watuhumiwa walijaribu kuwarubuni askari kwa kutoa rushwa ya Tsh. Milioni moja [1,000,000/=] ili waweze kuachiliwa  na wakati wanakamatwa walikuwa na pesa Tsh.laki tano[500,000/=] lakini askari walikataa hongo ya rushwa hiyo  na waliwakamata pamoja na pesa yao  na kuwafikisha kituoni na watafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine kamanda Muroto amesema Jeshi hilo limekamata nyara za Serikali  ambapo mnamo Tarehe 21,10,2019 majira ya saa 1:30 jioni  huko kijiji na kata ya MKOKA Tarafa ya ZOISA Wilaya ya KONGWA  Mkoani Dodoma  alikamatwa STEPHANO MTAGWA  KOGANI[39] Mkazi wa kijiji cha SONGAMBELE na HAMIS MATHAYO  MABUKU [45] na mkazi wa kijiji cha MATONGOLO  Wakiwa na pembe moja ya tembo   ndani ya mfuko wa Salfeti kiroba  kinyume cha sheria na watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Tukio jingine Kamanda Muroto amesema ni la kuvunja nyumba mchana na kuiba ambapo amekamatwa ELIAS SHABAN JOSEPH [21]Mkazi wa Mailimbili Mnadani   baada ya kuvunja nyumba mchana na kuiba maboksi 8 ya mafuta ya kupaka  na maboksi 4 ya pipi  mali yenye thamani ya TSH.720,000 Maeneo ya IPAGALA WEST  Dodoma  mali ya Willy Fidelis  Mgeni huku pia wakikamatwa wengine walioshiriki uhalifu huo .

Hata hivyo,Kamanda Muroto ameipongeza vyombo vya habari kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuuhabarisha umma.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post