WAZIRI WA ULINZI DK HUSSEIN MWINYI AKERWA NA USIMAMIZI USIORIDHISHA UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA USHETU


Waziri wa Ulinzi Dk Husein Mwinyi akipokea maelezo ya mradi kutoka kwa mkandarasi kampuni ya Mzinga Holding Meneja wa shirika la Mzinga na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mzinga holdings Meja Jenerali Seif Makona.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akimuongoza Waziri wa Ulinzi Dk Husein Mwinyi kuelekea eneo la Mradi
Mafundi wakiendelea na kazi katika eneo la ujenzi wa jengo hilo

Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog
Waziri wa Ulinzi, DK Husein Mwinyi amezitaka pande tatu zinazohusika na usimamizi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati uliopangwa kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma.

Waziri Mwinyi ametoa leo agizo hilo katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha, Wakala wa ujenzi Tanzania (TBA), Halmashauri ya Ushetu, na mkandarasi Mzinga holding baada ya kubaini upande hizo kulaumiana katika utekelezaji wa ujenzi huo na kusababisha mpaka sasa ujenzi huo kufikia asimia 27 badala ya asilimia 50 kwa mujibu wa mkataba.

Amesema Serikali haitavumilia kuona ujenzi wa jengo hilo ukiendelea kwa kusuasua hali ambayo inaweza kusababisha kutokamilika kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza huku wasimamizi wakuu wa mradi huo wakiendelea kulaumiana bila sababu ya Msingi.

Waziri Mwinyi amesema serikali imebaini kuwepo kwa utolewaji wa vibali vya ujenzi kutoka kwa wakala wa Ujenzi TBA usioridhisha sanjari ucheleweshwaji wa utolewaji wa fedha kutoka Halmashauri hiyo kwenda kwa Mkandarasi Mzinga holding ambayo ipo chini ya wizara yake.

Kwa upande wake mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amesema utendaji kazi wa TBA katika mradi wa ujenzi huo hauridhishi na umesababisha kusuasua kwa mkandarasi katika ujenzi huo licha ya serikali kutoa shilingi bilioni 9.1 lakini wao kama wasimamizi wakuu wa mradi huo wamekuwa hawaonekani katika eneo la ujenzi na kusababisha mkandarasi kushindwa kufanya kazi.

Naye Kaimu meneja wa TBA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Sobe Makonyo amesema wameshakubaliana na kampuni ya Mzinga Holdings kujenga jengo hilo kwa saa 24 na ujenzi wake utamilka kwa wakati kama vile mkataba unavyoekeza na watahakikisha wanaweka watumishi wao katika eneo la maradi.

Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Atanas Lucas amesema halmashauri hiyo ilipokea fedha kutoka serikali kuu shilingi bilioni 1.9 za wali ili kutekeleza mradi huo ambao unatajia kutumia shilingi bilioni 5.2

Atolea Ufafanuzi kuhusiana na Ujenzi huo Meneja wa shirika la Mzinga na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mzinga holdings Meja Jenerali Seif Makona amesema watahakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kuiomba TBA na Halmashauri ya Ushetu kutokwamisha vibali vya ujenzi na Malipo kwao.

Ujenzi wa jengo hilo unatarajia kutumia shilingi bilioni 5.2 na Mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 27 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2 mwaka 2020.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post