MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA 2019 KUFANYIKA MKOANI SINGIDA

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini hapa leo, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa 2019 yanayo tarajiwa kuanza kufanyika mkoani Singida kuanzia kesho. 
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na Waandishi wa habari ukiendelea.





Na Dotto Mwaibale, Singida

MAADHIMISHO ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Singida ambapo Tanzania itaungana na nchi wanachama wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) katika kusherehekea siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema 
Nchimbi alisema mgeni rasmi katika maadhimisho hayoanatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kuwa yatazinduliwa kesho katika Uwanja wa Bombadia.

"Ndugu Wananchi napenda kuwafahamisha kuwa mkoa wetu
wa Singida umepewa heshima na Taifa kuwa mwenyeji wa Siku ya ChakulaDuniani.Maadhimisho haya yatazinduliwa kesho Oktoba 10, 2019 natoa wito kwawananchi wa Singida na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja waBombadia ambako maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia kesho na kufikia kilele
chake Oktoba 16, 2019.

Dkt. Nchimbi alisema kaulimbiu ya maadhimisho hayo  inasema “Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa” na kuwa kauli mbiu
hiyo inalenga kuhamasisha jamii na wadau wote wa sekta kilimo kuchangia katikakuhakikisha nchi na dunia inakuwa na chakula cha kutosha wakati wote.

Alisema Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaonyesha hali ya
upatikanaji chakula mwaka 2019/2020 ni nzuri, kwani nchi, ina chakula cha kutosha. Kiwango cha utoshelevu wa chakula ni asilimia 119. Uzalishaji wa mazao ya chakula ulifikia tani 16,408,309 ukilinganisha na mahitaji ambayo ni
tani  13,842,536. 


Kati ya hizo Tani9,007,909 ni mazao ya nafaka na tani 7,400,400 ni mazao yasiyonafaka.Tunawapongeza watanzania kwa kutekeleza kauli mbiu hii kwa vitendo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527