WATU NANE WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI KUTUMBUKIA MTONI TANGA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, October 26, 2019

WATU NANE WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI KUTUMBUKIA MTONI TANGA

  Malunde       Saturday, October 26, 2019Watu nane wamefariki dunia wilayani Handeni mkoani Tanga, baada ya gari walilokuwa wanasafiria, kutumbukia mtoni kutokana na daraja kukatika. 

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, leo tarehe 26 Oktoba 2019, Edward Bukombe, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, amesema anafuatilia tukio hilo. 

Kamanda Bukombe amesema yuko njiani kuelekea eneo la tukio, na kwamba atatoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo, pindi atakapofika eneo la tukio.

“Hizo taarifa nimezipata na sasa hivi niko barabarani naelekea eneo la tukio, nikifika nitawajulisha kilichotokea. Maana kwa sasa niko mbali na tukio,” amesema Kamanda Bukombe.

Chanzo- Mwana Halisi Online
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post