WAZIRI WA MADINI - KILA MMOJA ATIMIZE WAJIBU WAKE

Na Issa Mtuwa - Geita

Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka Wachimbaji wa madini nchini kutimiza wajibu wao kwakuwa serikali imeshatimiza na inaendelea kutimiza wajibu wake kwa wachimbaji na wadau wengine wote katika sekta ya madini.


Hayo ameyasema  tarehe 14/09/2019 katika siku yake ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita wakati akiongea na wachimbaji wa madini ya ujenzi eneo la Katoro. 

Akiwa njiani kuelekea Bukombe Biteko aliongea na wachimbaji hao kwa kuwasisitiza kulipa kodi ya serikali na tozo nyingine kama sehemu ya kutimiza wajibu wao na kuunga mkono maamuzi ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli aliewasikiliza kiliochao kuhusu utitiri wa kodi zilizokuwa kero kwa wachimbaji na Rais kuamua kuziondoa. 

Biteko amewaambia wachimbaji madini kote nchini kuwa, kwa sasa ni zamu yao kutimiza wajibu kwa kulipa kodi, kuunga mkono jitihada alizo zionyesha Rais Magufuli zilizopelekea mageuzi makubwa katika sekta madini.

Wakati huo huo Biteko ambae pia ni Mbunge wa Bukombe ameungana na Waziri wa Nishati  Dkt. Medard Kalema katika kukagua utekelezaji wa ilani ya chama tawala katika jimbo la Bukombe katika usambazaji wa umeme kwa wananchi. Pamoja na kusikiliza kero za wana Bukombe kuhusu Umeme Mawaziri hao wamejionea kusua sua kwa usambazaji wa umeme na hatua iliyofikiwa jambo lililopelekea kung’olewa kwa Meneja wa Tanesco wilaya ya Bukombe kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake.

“Mhe. Kalemani leo mimi sina cha kuongea ujio wako wana Bukombe wanasubiri kusikia kutoka kwako umeme utawaka lini, kwani wamekuwa wakikuona kwenye vyombo vya habari mara  Kilimanjaro, Mara Songea, Mara Tanga ukipita ukiwasha umeme Wanabukombe nao leo wanapenda wakuone ukiwasha umeme hapa kwao” alisema Biteko Mbunge wa Bukombe huku akishangiliwa na umati mkubwa wa Wananchi wa Bukombe.

Nae Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alijibu mapigo ya mbunge wa Bukombe kwa kutolea majibu kero zote zilizowasilishwa na Biteko kwa niaba ya wananchi wake.

“Mhe. Waziri, kwanza nikupongeze kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya kwa wananchi wako. Pili, nimekuja hapa mara mbili na leo mara ya tatu maagizo niliyoyatoa awali naona hayajatekelezwa, sasa nasema hivii, Meneja wa Tanesco wilaya ya Bukombe kuanzia sasa namfuta kazi sio Meneja tena  wa hapa Meneja wa Kanda tafuta kwa kumpeleka hapa lete mwingine kesho”

“Pale sokoni kesho, nasema kesho, ipelekwe Transformer na jioni saa 10 umeme uwake kwenye maduka ya wafanyabiashara.  Mkandarasi naagiza ifikapo Desemba mwaka huu vijiji vyote 72 vya wilaya ya Bukombe viwe vimesha unganishwa umeme. Mhe. Biteko mimi sijaja kukaa sana hapa yangu ni hayo na kama haya yote niliyo yaangiza kwa kila jambo yasipotekelezwa kwa tarehe zilizo pangwa nipigie simu” alisisitiza Kalemani wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Jimbo la Bukombe.

Kwa upande mwingine Dkt. Kalemani amemsifu Mbunge wa Bukombe ambae ni Waziri wa Madini kwa kutoa vifaa 250 bure  vya kuunganishia umeme huku kila kimoja kikigharimu Tshs. 300,000 kila kimoja itakacho fungwa kwenye nyumba ya ukubwa wa chumba na sebule.

Biteko yupo kwenye ziara ya kikazi katika mikoa ya Geita, Kilimanjaro na Kagera.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527