KAMPENI YA NYUMBA NI CHOO YAFUNGWA....WASIO NA VYOO KUPIGWA FAINI SHINYANGA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati akifunga kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira maarufu kama nyumba ni choo
Na Salvatory Ntandu - Malunde 1 blog
Baada ya mkoa wa Shinyanga kubainika kuwa na kaya zisizokukwa na vyoo 7100, Serikali imesema itaanaza kuawachukulia hatua kali za kisheria watu watakaobainika kutokuwa na vyoo kwa kuwatoza faini ya shilingi laki tano ifikapo Disemba 31 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati akifunga kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira maarufu kama nyumba ni choo iliyofanyika kwa mikoa sita ya kanda ya ziwa iliyofanyika wilayani Kahama.

Amesema ni lazima mkoa huo ufikie asilimia 100 ya ujenzi wa vyoo bora kabla ya Disemba 31 mwaka huu hivyo tayari maagizo yameshatolewa kwa viongozi wa ngazi zote juu ya namna ya kutekeleza agizo hilo kwa wananchi ili kuhakikisha suala la ujenzi wa vyoo linapatiwa ufumbuzi wa haraka.

“ Shinyanga ni mkoa tajiri sana kwa kuwa rasilimali nyingi za madini aina ya dhahabu, almasi na mazao mbalimbali hivyo ni aibu kusikia bado kuna kaya ambazo hazina vyoo na wakazi wake wanaendelea kujisaida vichakani licha ya kupatiwa elimu juu ya ujenzi wa vyoo bora na serikali”alisema Telack.

Sambamba na hilo Telack amewaagiza wakuu wote wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kuhakikisha wananunua sabuni na ndoo za kuwekea maji kwaajili ya wanafunzi kunawa mikono baada ya kutoka vyooni ili kuzuia kupata bacteria wanapotoka vyooni.

Kwa upande wake mratibu wa kampeni ya Taifa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Anyitike Mwakitalima amesema takwimu za ujenzi wa vyoo bora zinaonyesha kuwepo kwa mwamko wa watu kujenga vyoo katika mkoa ambayo wameitembelea baada ya uhamasishaji huo

“uhamasishaji huo katika mikoa ya kanda ya ziwa timu ya uhamasishaji inayoongozwa na Mrisho Mpoto itaelekea katika mikoa mingine ambayo bado ina changamoto yavyoo lengo likiwa ni kuzifikia Halmashauri zote nchini” alisema Mwakitalima.

Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira maarufu kama ‘Nyumba ni Choo’kwa kanda ya ziwa katika imetembelea halmashauri 43, kata 181 na vijiji 877 kati ya 4,400 katika mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga na ilianza Mei 25 mwaka huu mkoani Kagera.

Mratibu wa kampeni ya Taifa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Anyitike Mwakitalima akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527