EMMA MARIE : NI LAZIMA WANAUME WASHIRIKISHWE KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 25, 2019

EMMA MARIE : NI LAZIMA WANAUME WASHIRIKISHWE KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA

  Malunde       Wednesday, September 25, 2019

Imeelezwa kuwa ili kufikia usawa wa kijinsia nchini Tanzania ni lazima wanaume washirikishwe kwenye masuala yanayohusu wanawake.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wanawake nchini Rwanda 'Pro-Femmes/TH', Emma Marie Bugingo leo Septemba 25,2019 wakati  akizungumza kwenye Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam.

Bugingo alisema mabadiliko ya kweli kufikia usawa wa kijinsia yatafanikiwa endapo wanaume watakuwa bega kwa bega na wanawake.

Aidha aliwahamasisha wanawake washiriki kwenye utungaji wa sheria mbalimbali na kuhakikisha sheria hizo zinatafsiriwa kwa lugha rahisi ili kila mwanamke bila kuwasahau walioko pembezoni wawe na uwezo na utashi wa sheria hizo.

"Ni lazima tukubaliane kuwa binadamu wote ni sawa na kwamba mfumo dume unadhoofisha wote wanawake na wanaume. Ili kufikia mabadiliko ya kweli ni lazima wanawake na wanaume tushirikiane,tushikamane na tuwe na nguvu moja",alisema.

"Nchini Rwanda tumefanikiwa kufikia usawa wa kijinsia kutokana na uwepo wa sheria zisizogandamiza wanawake. Lakini pia tumefanikiwa kutokana na Viongozi wetu akiwemo Rais Paul Kagame kuwa na utashi wa kisiasa kwamba ili kufikia maendeleo ya kudumu ni lazima tuwashirikishe wanawake",aliongeza.

Naye Mwanaharakati kutoka nchini Kenya Njoki Njehu aliwataka wanawake kuondokana na dhana ya kuwezeshwa na kubainisha kuwa kinachotakiwa ni vikwazo vinavyogandamiza wanawake viondolewe.

Kwa upande wake,Mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka Mbeya,Florah Mathias Mlowezi alisema mabadiliko ya kweli pia yanapaswa kuanzia kwa mtu binafsi hivyo kuwataka wanawake kutokata tamaa pale wanapokumbana na changamoto za kupigania haki za wanawake.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wanawake nchini Rwanda 'Pro-Femmes/TH', Emma Marie Bugingo akizungumza leo Septemba 25,2019 kwenye Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka Mbeya,Florah Mathias Mlowezi,Kulia ni Mwanachama wa TGNP Mtandao, Usu Mallya- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wanawake nchini Rwanda 'Pro-Femmes/TH', Emma Marie Bugingo akizungumza kwenye Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam.
Wa pili kulia ni Mwanaharakati kutoka nchini Kenya Njoki Njehu akizungumza kwenye Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam. 
Mwanachama wa TGNP Mtandao, Usu Mallya akizungumza kwenye Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam. 
Mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka Mbeya,Florah Mathias Mlowezi akizungumza kwenye Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam. 
Washiriki wa Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' wakifurahia burudani ya muziki katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' wakifurahia burudani ya muziki katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' wakifurahia burudani ya muziki katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Tamasha la 14 la Jinsia 'Gender Festival 2019' wakifurahia burudani ya muziki katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post