CCM BUKOBA YANG'OA VIJANA 15 WA VYAMA VYA UPINZANI


 Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kagera Mhe. Hamimu Mahamud akimpokea aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji Rwagati Deodati Christian (CHADEMA) 

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Vijana 15 kutoka vyama vya upinzani vya CHADEMA na ACT Wazalendo katika kata ya Kemondo Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji Kigarama kijiji Rwagati Deodati Christian wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Vijana hao wamehamia CCM Septemba 25, 2019 katika sherehe za maadhimisho ya Halmashauri ya Bukoba ya Kijani yaliyofanyika katika ofisi ya kata Kemondo mkoani Kagera yenye lengo la kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM na kuhimiza vijana kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Vijana hao akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji Kigarama kijiji Rwagati Deodati Christian wamesema kuwa ni kazi kubwa aliyoifanya Rais Magufuli katika kuibadilisha nchi katika mfumo mpya ki maendeleo na wao kupenda harakati zake hivyo kuwa na shauku ya kurejea ndani ya chama hicho kujifunza na kuhamasisha maendeleo kwa vijana wenzao.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi halmashauri ya wilaya ya Bukoba Paulo Mwita amewataka vijana hao kufuata misingi sheria na kanuni za chama hicho kama ambavyo wamekikuta chama hicho.

Akiwapokea vijana hao Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kagera Mhe. Hamimu Mahamud amewataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri katika kuleta amani na maendeleo ndani ya chama hicho huku akiwataka viongozi wa chama hicho kiwapokea vizuri na kuwaelekeza misingi ya chama hicho.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji Rwagati Deodati Christian (CHADEMA) akielezea sababu za kujiunga CCM
Vijana wakila kiapo baada ya kuhamia CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527