PPRA YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KUHUSU MFUMO WA TANePS


 Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, kabla ya Ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo ya TANePS, jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, akizungumza wakati wa ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo kuhusu Mfumo wa TANePS jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS
****
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqqaro, amefungua awamu ya nne ya  mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa Njia ya Mtandao (TANePS) kwa wataalam wa manunuzi na Tehama kutoka taasisi nunuzi. 

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo wapatao 172 kutoka taasisi nunuzi 65, Mh.  Daqqaro alipongeza jitihada za Serikali kwa kuanzisha mfumo huo mpya wa  TANePS unaosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma - PPRA kwa kuwa utasaidia kupunguza malalamiko na kero zilizokuwa zinaelekezwa  kwenye sekta ya manunuzi ya umma ikiwemo kukabiliana na vitendo vya  rushwa, kupunguza gharama na muda wa michakato ya manunuzi.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa Mfumo huo utaisaidia Serikali kuokoa  fedha nyingi ambazo zinaelekezwa kwenye sekta hiyo ya manunuzi, na kutoa wito kwa wadau wote wa manunuzi ya umma kutoa ushirikiano wa dhati ili mfumo huo ufanye kazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post