TETESI ZA SOKA LEO ALHAMIS SEPTEMBA 26,2019

Christian Eriksen
Real Madrid inamtaka kiungo wa kati wa Tottenham raia wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, kusaini mkataba wa awali mwezi Januari - na baadae atahamia Spurs kwa meneja Mauricio Pochettino. (Mirror)

Tottenham wanahofia Eriksen atakataa mapendekezo ya kumuuza mwezi Januari , hii ikimanisha kuwa anawza kuondoka kwa uhamisho usio na malipo msimu ujao. (Mail)

Mshambuliaji wa timu ya Juventus Mario Mandzukic alikataa euro milioni 7 alizopewa kwa mwaka kuichezea timu ya Qatar kwa hiyo Mcroatia huyo mwenye umri wa miaka 33 ana fursa ya kujiunga na Manchester United mwezi Januari mwaka ujao. (Mail)Mario Mandzukic alikataa euro milioni 7 alizopewa na Qatar

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amejiandaa kumthamanisha mchezaji Harry Kane, mwenye umri wa miaka 26 katika kiwango cha thamani ya euro milioni 250 , kwa lengo la kuendelea kubaki na mshambuliaji huyo wa England hadi mwisho wa kile kinachoweza kuwa ni msimu mwingine Spurs kukosa kombe. (Telegraph)

Boca Juniors wametoa ofa yao ya kutaka kusaini mataba na mchezaji wa safu ya mashambulizi Mswiden Zlatan Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 37, kutoka LA Galaxy. (AS)Totttenham yaazimia kumtahamanisha Harry Kane kwa kiwango cha thamani ya euro milioni 250

Mshambuliaji wa RB Salzburg raia wa Norway Erling Braut Haaland, mwenye umri wa miaka 19, amedokeza kuwa atahamia katika Primia Ligi baada ya kufunga mabaoi matatu katika gemu moja katika mchezo wa Championi Ligi . (mail)Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling

Meneja wa zamani ya klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 28, amemuambia kuwa anatakiwa kujiunga na Paris St-Germainikiwa anataka kushinda Championi Ligi . (Het Nieuwsblad via Sun)

Mchezaji mashuhuri wa Barcelona Xavi, ambaye kwa sasa ni kocha wa Qatar, anamuona mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, mwenye umri wa miaka 24, kama mchezaji anayefaa kusaini mkataba nae ikiwa wakati mmoja ataiongoza Nou Camp. (Mail)Kevin de Bruyne amemuambia mshambuliaji wa RB Salzburg raia wa Norway Erling Braut Haaland, anatakiwa kujiunga na Paris St-Germainikiwa anataka kushinda Championi Ligi

Makamu mwenyekiti mtendaji wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na Glazers kuhusu kufanya mabadiliko ya kile alichokitaja kama 'utamaduni ' katika klabu hiyo. (Express)

Barcelona wanataka kuhakikisha kwamba kiungo wa safu ya mashambulizi Ansu Fati mwenye umri wa miaka 16 hasafiri kuelekea katika michuano ya Kombe la dunia la vijana walio chini ya umri w amiaka 17 ili aweze kucheza gemu dhidi ya mahasimu wao Real Madrid tarehe 26 Oktoba. (Marca)

Manchester United walilazimika kumtafuta kiungo wa kati Peter Thomas kutoka Rochdale ambaye alikuwa mchezaji wa ziada ambaye hatimae hakutumiaka kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Carabao Cup katika kipindi cha dakika 15 pekee (Sun)Ole Gunnar Solskjaer anasema kutompa unahodha wa Manchester United hakuna uhusiano wowote na taarifa za Pogba kuihama timu

Uamuzi wa Ole Gunnar Solskjaer wa kutompa kiungo wa kati Paul Pogba fursa ya kuwa na nahodha wa Manchester United hauna uhusiano wowote na taarifa za kuhusishwa uhamisho wa Mfaransa huyo - ilikuwa ni kwasababu Axel Tuanzebe alikulia katika Rochdale. (Mirror)
Mshambulizi wa Juventus wa miaka 33 Mcroatia Mario Mandzukic

Manchester United inapania kumsajili mshambulizi wa Juventus wa miaka 33 Mcroatia Mario Mandzukic na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na Barcelona Ousmane Dembele, 22, Januari Mwakani. (The Independent)

Maafisa wa matibabu wa mshambuliaji wa Newcastle na England Andy Carroll, 30, wanahofia mchezaji huyo huenda isiingie uwanjani hadi baada ya Krismasi japo anaendelea kupata nafuu kufuatia jaraha la mguu alilopata. (Telegraph)Jurgen Klopp, Kocha wa Liverpool

Manchester United inafuatilia mchezo wa kiungo wa kati wa Italia wa miaka 19 Sandro Tonali atashiriki mechi ya Brescia dhidi ya Juventus siku ya Jumanne. (Mail)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema meneja wa sasa wa Rangers na nahodha wa zamani wa Reds Steven Gerrard ndiye atakayemrithi atakapiamua kuondoka Anfield. (FourFourTwo)

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, bado anataka kuondoka Crystal Palace na anapania kushinikiza uhamisho dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa tena mwezi Januari Mwakani. (Calciomercato)Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha

Sevilla iko tayari kumuachilia kiungo wa kati wa Ureno Rony Lopes mwezi January, huku Newcastle ikimfuatilia mkufunzi huyo wa zamani wa Manchester City wa miaka 23. (Gol Digital via Chronicle)

Mshambuliaji wa zamani wa Celtic na Manchester United Henrik Larsson huenda akapewa wadhifa wa Southend, kutokana na hali ngumu ya kiuhchumi inayomkabili na ukosefu wa tajiriba ya ukufunzi wa vilabu vya Uingereza ambao umekua changamoto kwake . (Sky Sports)

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino amegusia kuwa klabu hiyo itakuwa na shughuli nyingi mwezi Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa huku wakijiandaa kwa mchuano wa kombe Carabao Cup dhidi ya Colchester inayoshiriki soka ya daraja la pili. (Express).
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527