TETESI ZA SOKA LEO JUMATANO SEPTEMBA 25,2019 | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 25, 2019

TETESI ZA SOKA LEO JUMATANO SEPTEMBA 25,2019

  Malunde       Wednesday, September 25, 2019
Mshambulizi wa Juventus wa miaka 33 Mcroatia Mario Mandzukic

Manchester United inapania kumsajili mshambulizi wa Juventus wa miaka 33 Mcroatia Mario Mandzukic na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na Barcelona Ousmane Dembele, 22, Januari Mwakani. (The Independent)

Maafisa wa matibabu wa mshambuliaji wa Newcastle na England Andy Carroll, 30, wanahofia mchezaji huyo huenda isiingie uwanjani hadi baada ya Krismasi japo anaendelea kupata nafuu kufuatia jaraha la mguu alilopata. (Telegraph)

Manchester United inafuatilia mchezo wa kiungo wa kati wa Italia wa miaka 19 Sandro Tonali atashiriki mechi ya Brescia dhidi ya Juventus siku ya Jumanne. (Mail)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema meneja wa sasa wa Rangers na nahodha wa zamani wa Reds Steven Gerrard ndiye atakayemrithi atakapiamua kuondoka Anfield. (FourFourTwo)Jurgen Klopp, Kocha wa Liverpool

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, bado anataka kuondoka Crystal Palace na anapania kushinikiza uhamisho dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa tena mwezi Januari Mwakani. (Calciomercato)

Sevilla iko tayari kumuachilia kiungo wa kati wa Ureno Rony Lopes mwezi January, huku Newcastle ikimfuatilia mkufunzi huyo wa zamani wa Manchester City wa miaka 23. (Gol Digital via Chronicle)Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha

Mshambuliaji wa zamani wa Celtic na Manchester United Henrik Larsson huenda akapewa wadhifa wa Southend, kutokana na hali ngumu ya kiuhchumi inayomkabili na ukosefu wa tajiriba ya ukufunzi wa vilabu vya Uingereza ambao umekua changamoto kwake . (Sky Sports)

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino amegusia kuwa klabu hiyo itakuwa na shughuli nyingi mwezi Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa huku wakijiandaa kwa mchuano wa kombe Carabao Cup dhidi ya Colchester inayoshiriki soka ya daraja la pili. (Express).Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, akiwapa maelezo wachezaji wake

Mkurugenzi mkuu wa Arsenal Vinai Venkatesham amesema kuwa klabu hiyo huenda isawajili wachezaji wapya mwezi Januari wakati wa uhamisho wa wachezaji. (standard)

Meneja wa Newcastle Steve Bruce ana mpango wa kumtoa katika kikosi cha kwanza mshambuliaji wa Paraguay forward Miguel Almiron aliyejiunga na klabu hiyo mwezi Januari kwa £20m. (star)
Tetesi Bora Jumanne

Manchester United wameanzisha mazungumzo na kiungo wa kati Paul Pogba kuhusu mkataba mpya. Pogba mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa amebakiza miaka miliwi katika mkataba wake wa sasa. (Times)Kiungo wa kati wa Manchester United, Paul Pogba

Real Madrid wanafuatilia kwa karibu hali ya baadae ya uhamisho wa mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester City na England Raheem Sterling,mwenye umri wa miaka 24, ambaye alifunga magoli saba katika michezo minane kwa klabu na nchi yake msimu huu. (El Mundo Deportivo - in Spanish)

Mshambuliaji wa Chelsea Mbrazil Willian anafuatiliwa kwa karibu na timu ya Juventus, ambao wanaweza kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31- wakati mkataba wake utakapomalizika msimu ujao . (Sky Sports via Tuttosport)Mshambuliaji wa Chelsea Mbrazil Willian anafuatiliwa kwa karibu na timu ya Juventus,

Liverpool wanakaribia kukamilisha mkataba wa mavazi ya kimichezo na watengenezaji wa jezi Nike kuanzia msimu ujao. (Telegraph)

Chelsea wanayo matumaini ya kumuajili kiungo wa mashambulizi wa kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Fikayo Tomori, mwenye umri wa miaka 21, na inatumainiwa kuwa atasaini mkataba wa miaka mitano katika wiki chache zijazo. (La Gazzetta dello Sport)AC Milan wanamlenga mlinzi wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier kwa uhamisho.

AC Milan wanamlenga mlinzi wa Tottenham mwenye umri wa miaka 26 kutoka Ivory Coast Serge Aurier kwa uhamisho. (Sport Mediaset via Teamtalk)

Manchester United wanatarajiwa kutangaza rekodi ya mapato yao ya mwaka ambayo yatakuwa makubwa kwa kiwango cha pauni milioni 615 zaidi Jumanne. (ESPN)

Aston Villa na West Brom wanamtaka kiungo wa safu ya nyuma -kushoto ya England Muingereza Sam McCallum mwenye umri wa miaka 19 . (Football Insider)Chelsea wanayo matumaini ya kumuajiri kiungo wa mashambulizi wa kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Fikayo Tomori

Mshabiki wa Chelsea wanasema kuwa kuondolewa kwa bango la Eden Hazard kabla ya gemu dhidi ya Liverpool lilikuwa ni kosa kwani klabu hiyo iliwapatia mashabiki mabango yasiyofaa kujonyesha.(Standard)

Peterborough United wamewapatia ofa watumishi wa kampuni ya ndege ya Thomas Cook tiketi za bure za kutazama mchezo wa Jumamosi dhidi ya AFC Wimbledon kufuatia kufilisika kwa kampuni hiyo ya safari ambayo ina makao makuu katika mji huo . (Mail)
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post