TETESI ZA SOKA LEO JUMANNE SEPTEMBA 24,2019

Real Madrid wanafuatilia kwa karibu hali ya baadae ya uhamisho wa mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester City na England Raheem Sterling

Real Madrid wanafuatilia kwa karibu hali ya baadae ya uhamisho wa mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester City na England Raheem Sterling,mwenye umri wa miaka 24, ambaye alifunga magoli saba katika michezo minane kwa klabu na nchi yake msimu huu. (El Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester United wameanzisha mazungumzo na kiungo wa kati Paul Pogba kuhusu mkataba mpya. Pogba mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa amebakiza miaka miliwi katika mkataba wake wa sasa. (Times)

Liverpool wanakaribia kukamilisha mkataba wa mavazi ya kimichezo na watengenezaji wa jezi Nike kuanzia msimu ujao. (Telegraph)Pogba anatarajia kusaini mkataba mpya na Manchester United

Barcelona wanaangalia uwezekano wa kusaibni mkataba na winga wa Reign FC Megan Rapinoe mwenye umri wa miaka 34. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani alishinda tuzo ya mwanasoka bora mwanamke katika Tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mjini Milan Jumatatu. (ESPN)

Mshambuliaji wa timu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen Kai Havertz, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia katika timu za Manchester United, Arsenal na Chelsea, amethamanishwa kwa kiwango cha pauni 90 . Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20-alishinda magoli 17 katika michezo 34 ya Ligi ya Ujerumani - Bundesliga (Sun)

West Ham imewezesha kusitisha mipango ya kupata haki ya mkataba wa kuupatia jina uwanja wa London Shadi kufikia mwisho wa msimu. (Football Insider)Mshambuliaji wa timu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen Kai Havertz, amethamanishwa kama mchezaji mwenye thamani ya pauni milioni 90

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, mwenye umri wa miaka 46, ni mtu wa pili miongoni mwa watu wanaoweza kufukuzwa katika Primia Ligi - baada ya meeneja wa Everton Mreno Marco Silva. (Sun)


Mshambuliaji wa Chelsea Mbrazil Willian anafuatiliwa kwa karibu na timu ya Juventus, ambao wanaweza kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31- wakati mkataba wake utakapomalizika msimu ujao . (Sky Sports via Tuttosport)Mshambuliaji wa Chelsea Mbrazil Willian anafuatiliwa kwa karibu na timu ya Juventus,

Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya Juventus Mcroatia Mario Mandzukic, mweney umri wa maika 33, ana matumaini ya kupata nafasi katika Primia Ligi mwezi Januari. (Tuttosport - in Italian)

Chelsea wanayo matumaini ya kumuajili kiungo wa mashambulizi wa kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Fikayo Tomori, mwenye umri wa miaka 21, na inatumainiwa kuwa atasaini mkataba wa miaka mitano katika wiki chache zijazo. (La Gazzetta dello Sport)AC Milan wanamlenga mlinzi wa Tottenham mwenye umri wa miaka kutoka Ivory Coast Serge Aurier kwa uhamisho.

AC Milan wanamlenga mlinzi wa Tottenham mwenye umri wa miaka kutoka Ivory Coast Serge Aurier kwa uhamisho. (Sport Mediaset via Teamtalk)

Manchester United wanatarajiwa kutangaza rekodi ya mapato yao ya mwaka ambayo yatakuwa makubwa kwa kiwango cha pauni milioni 615 zaidi Jumanne. (ESPN)

Aston Villa na West Brom wanamtaka kiungo wa safu ya nyuma -kushoto ya England Muingereza Sam McCallum mwenye umri wa miaka 19 . (Football Insider)Chelsea wanayo matumaini ya kumuajili kiungo wa mashambulizi wa kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Fikayo Tomori

Mshabiki wa Chelsea wanasema kuwa kuondolewa kwa bango la Eden Hazard kabla ya gemu dhidi ya Liverpool lilikuwa ni kosa kwani klabu hiyo iliwapatia mashabiki mabango yasiyofaa kujonyesha.(Standard)

Peterborough United wamewapatia ofa watumishi wa kampuni ya ndege ya Thomas Cook tiketi za bure za kutazama mchezo wa Jumamosi dhidi ya AFC Wimbledon kufuatia kufilisika kwa kampuni hiyo ya safari ambayo ina makao makuu katika mji huo . (Mail)
Tetesi za soka Jumatatu

Kiungo wa kati wa zamani wa Barcelona Xavi, ambaye ni meneja wa timu ya Qatari ya Al-Sadd, anasema kuwa itakuwa ni tatizo kwake kuwaongoza wachezaji wenzake wa zamani kama vile Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets katika Nou Camp. (Ara, via Goal)Kiungo wa kati wa Barcelona Xavi, ambaye ni meneja wa timu ya Qatari ya Al-Sadd, anasema kuwa itakuwa ni tatizo kwake kuwaongoza Lionel Messi, Luis Suarez na Sergio Busquets

Roy Keane amesema kuwa "ameshtushwa na kusikitishwa " na namna klabu yake ya zamani Manchester United walivyoshindwa 2-0 na West Ham Jumapili. (Sky Sports, via Evening Standard)

Mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 26, aliyejiunga na timu hiyo ya Italia kutoka Manchester United msimu huu, anasema kuwa kocha wa klabu hiyo Antonio Conte ni mtu ambaye ''anamsaidia kila siku na humpa motisha''. (Metro)Mario Balotelli, anasema amefanya ''kazi kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopita

Meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho anasema golikipa wa Uhispania David de Gea, mwenye umrui wa miaka 28, alikuwa na "bahati kidogo'' kupata mkataba mpya mzuri na klabu hiyo . (Sky Sports, via Mail)

Mashabiki wapatao 1,000 wa timu ya Valencia waliandamana kabla ya mechi dhidi ya Leganes, kwa kutofurahishwa na namna mmiliki mwenza wa Salford City Peter Lim, na rais Anil Murthy anavyoendesha a klabu hiyo ya ligi ya La Liga . (Marca)

Mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli,ambaye anaweza kuchezea Brescia dhidi ya Juventus Jumanne , anasema amefanya ''kazi kubwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopita " kuliko'' kipindi cha muongo mzima wa kazi yake'' huku kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 akilenga kupata nafasi katika kikosi cha nchi hiyo kitakachocheza kombe la Euro 2020. (Football Italia).
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post