KAMPUNI BINAFSI YA ULINZI SGA YATOA MAFUNZO YA USALAMA BURE | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 28, 2019

KAMPUNI BINAFSI YA ULINZI SGA YATOA MAFUNZO YA USALAMA BURE

  Malunde       Saturday, September 28, 2019

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya SGA Security, Eric Sambu (kushoto) akizungumza jijini Dar Es Salaam leo wakati wa kuadhimisha miaka 35 ya kutoa huduma za ulinzi nchini. Kulia ni Meneja wa Wateja na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Aikande Makere.

Kampuni ya ulinzi, SGA Security, imetoa mafunzo ya bure ya usalama kama sehemu ya utoaji wa huduma kwa jamii na kuwazawadia watumishi wake wa muda mrefu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 35 ya kuwepo nchini Tanzania.

Wiki iliyopita kampuni hiyo ilitoa mafunzo kwa wateja wake wakubwa juu ya mbinu mbalimbali za kisasa za kupambana na changamoto za kiusalama.

Semina hiyo kwa wateja wake ilifanyika Ijumaa Septemba 27 jijini Dar es Salaam na mafunzo yaliongozwa na wataalam waliobobea kwenye masuala ya usalama ambapo zaidi ya mameneja 80 wa usalama wa makampuni makubwa na mabenki nchini walihudhuria.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa SGA, Eric Sambu, alisema kwamba kampuni hiyo ya ulinzi imeamua kutoa huduma kwa jamii kama sehemu ya kusheherekea mafanikio yake nchini.

SGA pia imetoa mafunzo ya usalama kwenye shule 12 za msingi mkoani Dar es Salaam ambapo wanafunzi zaidi ya 2,000 walinufaika. Mafunzo hayo yalikua juu ya majanga ya moto, huduma ya kwanza, mazingira, afya na usalama kwa ujumla.

Ikiwa ina watamushi zaidi ya 5,800, nchini Tanzania, SGA kwa sasa ndio kampuni kubwa ya ulinzi nchini.

Katika shughuli za kuadhimisha miaka 35 nchini, kampuni pia imeanzisha ‘Club 20’ ambao wanachama wake ni watumishi walioitumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20. 

SGA aliwatuza watumishi 16 waliotumikia kampuni kwa muda mrefu ambao pia wamefikia muda wa kustaafu.

Wakati huo huo, mwakilishi kutoka jeshi la polisi nchini ameipongeza SGA kwa kujali maslahi ya watumishi wake na kuongoza kwa mfano, akisema kwamba kampuni nyingi binafsi za ulinzi hazifuati miongozo iliyotolewa kuhusiana na mafunzo, usimamizi, ukaguzi na mishahara.

Amezitaka kampuni nyingine za ulinzi kuiga mfoano wa SGA.

Ikiwa ina waajiriwa zaidi ya 80 waliotumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20 kwenya biashara ya faida kubwa, SGA ina kila sababu ya kusherehekea, amesema Sambu. SGA pia ina watumishi takribani 2,200 walioajiriwa kwa zaidi ya miaka 10.

“SGA ni kampuni ya kwanza binafsi ya ulinzi kuingia Tanzania na imedhihirisha kwamba kuwajali watumishi wake ni muhimu kwa mafanikio ya kampuni,” Sambu amesema.
Watumishi wa SGA wakishiriki kwenye Siku ya Usafi Duniani kama sehemu ya kuadhimisha miaka 35 ya kuwepo nchini Tanzania

“Kampuni mama ina watumishi za ya 18,000 na suala la muhimu kwetu ni watu. Tumewekeza sana katika utoaji wa mafunzo na tunahakikisha kwamba mishahara yetu inaongoza kwenye soko kama sehemu ya kuwapa motisha watumishi wetu,” aliongeza.
Amesema kwamba kampuni anaadhimisha miaka 35 ya utoaji huduma nchini Tanzania huku ikiwa inakua siku hadi siku, hususan katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Ameeleza zaidi kwamba mafanikio ya kampuni yameletwa na watumishi wake ambapo amesema ni waaminifu, waadilifuna wachapa kazi kwa bidii.

“Matukio ya hivi karibuni kwenye mazingira ya kibiashara nchini yamekuwa kama fursa ya kujifunza na kuwawezesha wafanyakazi wetu kwenda sambamba na matakwa ya wateja,” ameongeza.

“Kila mara tunajipanga upya katika utendaji wetu, huku tukiwekeza kwenye teknolojia na watumishi wetu kuhakikisha kwamba hakuna jambo linaloharibika,” amesema Sambu.

SGA ni kampuni kongwe binafsi ya ulinzi Tanzania, ikiwa imeanza kazi mwaka 1984 kama Group Four Security. Inatoa huduma mbalimbali zikiwemo za walinzi, usalama wa kielektroniki, huduma za dharura na usafirishaji wa fedha.

“Tuna magari 224 na vituo 12 mikoani na watumishi wanaojituma, tuna miundombinu ya kutosha kuwahudumia wateja popote pale nchini,” Sambu amesema.

Menaja Rasilimali Watu wa SGA, Ebenezer Kaale, alisema kwenye tukio hilo kwamba watumishi wengi walioajiriwa kwa miaka mingi wanafanyakazi kwenye idara ya kusafirisha fedha, idara nyeti inayohitaji uadilifu na nidhamu ya hali ya juu.

Ikiwa ina mafanikio makubwa kwenye huduma za fedha, ambapo kampuni imehodhi asilimia 90 ya soko, watumishi kwenye idara wanastahili pongezi kwa mafanikio hayo.

Meneja wa Mahusiano ya Wateja, Aikande Makere, amesema kwamba kazi za SGA zitarahisishwa ikiwa wateja wanaenda na wakati kwa kufahamu mbinu za kisasa za kupambana na changamoto za kiusalama.

MwishoUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post