SERIKALI YAAGIZA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA WA SHINYANGA KUJENGA MAENEO YA MAEGESHO YA MALORI YA MIZIGO KABLA YA OKTOBA 25,2019 | MALUNDE 1 BLOG

Friday, September 20, 2019

SERIKALI YAAGIZA HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA WA SHINYANGA KUJENGA MAENEO YA MAEGESHO YA MALORI YA MIZIGO KABLA YA OKTOBA 25,2019

  Malunde       Friday, September 20, 2019

NA SALVATORY NTANDU

Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Shinyanga wametakiwa kujenga maaeneo ya maegesho ya malori ya mizigo na mafuta ambayo yemekuwa yakiengeshwa katika maeneo yasiyorasimi(makazi ya watu) hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa wananchi kabla ya octoba  25 mwaka huu.


Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kwenye kikao cha robo ya pili ya bodi ya barabara mkoa wa shinyanga, na kusema kuwa kumekuwa na tabia ya uegeshaji holela wa malori ya  katika makazi ya watu huku mengine yakiwa na kemikali hatari kama vile gesi na mafuta.

Amesema serikali haiwezi kukubali hali hiyo huku wenye mamlaka ya kusimamia na kupanga maeneo ya miji na wilaya wakiwa hawatimizi wajibu wao na kuendelea kuruhusu uegeshaji holela wa malori hayo ambao ni hatari kwa maisha  kwa uslama wa wananchi wa mkoa huo.

Amefafanua kuwa utengaji wa maeneo ya malori ya mizingo kwenye halmashauri za mkoa wa shinyanga kutaongeza mapato  kutokana na malori hayo na pia itawawezesha wamiliki wa malori hao kutoibiwa vifaa vyao vya magari katika vituo hivyo kwani  katika maeneo hayo kutakuwa na ulinzi wa kutosha.

Michael Matomora ni mkurugenzi wa Halamshauri ya Ushetu na Godfrey Mwangulumbi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga wamesema katika bajeti ya mwaka 2018/19 hawakutenga bajeti kwaajili ya kutenga maeneo hayo lakini kwa mwaka huu wa fedha watahakikisha agizo hilo linatekelezwa harasa.

Naye Kaimu Meneja wa TANROAD mkoa wa Shinyanga Mhandisi, Mibara Ndilimbi amesema kwa sasa Wakala  huo unaendelea kujenga eneo la maengesho la Kagonjwa Isaka ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi sambamba na kuboresha eneo la Maegesho la Mjini Kahama.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post